HISTORIA FUPI YA BASIL PESAMBILI MRAMBA .

HISTORIA FUPI YA BASIL PESAMBILI MRAMBA .

Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Pesambili Mramba mwenye uri wa miaka 81 amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency. Basil Pesambili Mramba alizaliwa Mei 15, 1940,alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Kwaleina Bush School mwaka 1948 na kuhamia

Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Marehemu Basil Pesambili Mramba.

Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Pesambili Mramba mwenye uri wa miaka 81 amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency.

Basil Pesambili Mramba alizaliwa Mei 15, 1940,alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Kwaleina Bush School mwaka 1948 na kuhamia katika Shule ya Msingi Shimbi alikosoma mpaka mwaka 1952. Mwaka 1953 alijiunga na Shule ya Mkuu Mission Primary School alikosoma mpaka mwaka 1954 na kuhitimu elimu ya msingi.
 
Mwaka 1955, alijiunga na Shule ya Sekondari Umbwe mpaka mwaka 1960. Mwaka 1961 alijiunga na Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora na kusoma kidato cha tano na sita na kuhitimu mwaka 1962 baada ya kuhitimu Mramba alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, Nchini Uganda ambako alisomea shahada yake ya kwanza katika masuala ya siasa kuanzia mwaka 1963 hadi 1967 na baadae alijiunga na Chuo Kikuu cha City University Graduate School cha London nchini Uingereza akisomea Shahada ya Uzamili na kuhitimu mwaka 1968.
 
Baada ya kuhitimu masomo yake Basil Pesambili Mramba aliajiriwa na Kampuni ya Williamson Diamond, Mwadui Shinyanga akiwa kama msaidizi katika masuala ya utawala, ajira aliyoendelea nayo mpaka mwaka 1969 na baadae alipata ajira katika Shirika la Maendeleo (NDC) akiwa kama mkurugenzi wa nguvukazi mpaka mwaka 1972. Wakati akiendelea na kazi, mwaka 1971 Mramba aliamua kujiendeleza kielimu, akajiunga na Chuo Kikuu cha Havard Business School cha nchini Marekani, akisomea cheti cha usimamizi wa biashara,Mwaka 1995 alijiunga na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) akiwa kama Mkurugenzi na akaendelea na kazi mpaka mwaka 1980.
 
Basil Pesambili Mramba aliingia kwenye siasa mwaka 1980 na kugombea Ubunge wa Jimbo la Rombo, akadumu mpaka mwaka 1987. Baadaye alirejea tena bungeni mwaka 1995, akateuliwa na Hayati Rais Benjamin William Mkapa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi aliyoishika mpaka mwaka 2000,akiwa bunge aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Fedha kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2005.
 
Mwaka 2006, aliteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu, mwaka huohuo oktoba 10,2006 akahamishwa wizara na kupelekwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko hadi mwaka 2008.
 
Mwaka 2015 Basil Pesambili Mramba na mwenzake, Daniel Yona walikamatwa na kushtakiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakituhumiwa kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kupitia misamaha ya kodi,kesi hiyo ilinguruma kwa muda mrefu na hatimaye, walikutwa na hatia kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia serikali hasara, wakahukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani na faini ya shilingi milioni tano .

Mramba, Yona receive pre-community service counseling
Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona wakitumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam.

Baada ya hukumu hiyo Basil Pesambili Mramba na mwenzake Daniel Yona walikata rufaa lakini Oktoba 2, 2015 Jaji Projest Rugazia alitupilia mbali rufaa yao lakini akawapunguzia adhabu kutoka kifungo cha miaka mitatu gerezani hadi miwili na kufuta faini ya fedha hizo,baada ya kutumikia sehemu ya kifungo chao gerezani, hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, iliwabadilishia adhabu na kuwataka kutumikia kifungo cha nje sambamba na kufanya usafi katika maeneo ya jamii na kupangiwa kutumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam kwa saa nne za kila siku.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »