CEO BANK YA KILIMO AAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUSAIDIA UFUGAJI SAMAKI

CEO BANK YA KILIMO AAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUSAIDIA UFUGAJI SAMAKI

Mkurugenzi wa bank ya kilimo TADB, Frank Mugeta amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuwazesha ukuaji wa sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha makundi ya vijana na wakinamama katika swala la ufugaji wa samaki ambao wanatajwa kuwa chachu ya maendeleo na ajara kwa watu wengi Mugeta amesema kutokana na ongezekeo la binadamu

Mkurugenzi wa bank ya kilimo TADB, Frank Mugeta amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuwazesha ukuaji wa sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha makundi ya vijana na wakinamama katika swala la ufugaji wa samaki ambao wanatajwa kuwa chachu ya maendeleo na ajara kwa watu wengi

Mugeta amesema kutokana na ongezekeo la binadamu katika maeneo mbalimbali nchini kumepelekea idadi ya samaki kupungua hasa katika bahari kuu, maziwa, mito na mabwawa hivyo mbadala pekee wa kuongeza idadi ya samaki ni kujikita katika uwekezaji wa ufugaji katika maeneo mbalimbali husasani kanda ya ziwa

“ni vema kama nchi tuangalie jinsi ambavyo tunaweza kuweka nguvu yetu kubwa Zaidi katika swala la ufugaji wa samaki, na tunapoenda kuwasaidia watu wanaoenda kufuga samaki tutaongeza tija kwa watu wengi ambao wanaweza kufuga na tutawapata kwa wingi tofauti na ilivyo sasa ambapo wamepungua sana kutokana na ongezeko la watu” amesema

Amesema katika maendeleo ya kilimo sekta ya uvuvi itapewa kipambele kwasababu inaajiri watu wengi hususani vijana na wakina mama ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia familia zao katika malezi na ukuaji wa uchumi wa famila zao

Dkt Rashid Tamatama ni katibu mkuu Uvuvi amesema kuwa tayari serikali imeshaanda mpango wa kuwawezesha wavuvi katika vikundi vya ushirika kwa kuwapatia mitumbo ya mashine itakayo wawezesha wavuvi kuvua kwenye maji ya kitaifa ili kukabiliana na upungufu wa samaki uliopo

Amesema kwa muda mrefu wavuvi wamekuwa wakipata mavuno kidogo kutokana na vitendea kazi duni hasa maeneo ya pwani ambapo hutumia vyombo vya kizamani kama mitumbwi na ngalawa na vichache kati ya hivyo ndio hutumia mashine ambapo pia huishia kuvua katika maji ya ndani yaani kilomita chahe kutoka ukanda wa bahari

“tutaviwezesha baadhi ya vikundi vya ushirika vilivyopo ukanda wa pwani kupata boti za kisasa ambazo zinahitaji wataalamu kuziendesha lakini hatutawaacha peke yao, watakuwa chini ya uangalizi wa serikali kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu ambapo pia ndani ya muda huo tutawasaidia kupatama injinia wao wa kumeneji injini” amesema

Amebainisha baada ya miaka miwili ya uangalizi serikali itahakikisha wavuvi watakuwa na masoko ya uhakika na fedha zitakuwa zimesharudi ambapo wavuvi wataruhusiwa kumiliki vyombo kwahiyo hii ni moja ya skimu ambayo inahitaji sana ushiriki wa taasisi za kifedha kama TADB katika kukuza uwekezaji

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »