WALIMU WENYE ULEMAVU WAELEKEZA KILIO CHAO SERIKALINI

WALIMU WENYE ULEMAVU WAELEKEZA KILIO CHAO SERIKALINI

Walimu wenye ulemavu wamesema wamekuwa wakikaliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo miundombinu kutokuwa rafiki kwao. Wakizungumza leo jijini Dodoma katika kongangano lililowakutanisha walimu wenye ulemavu Tanzania, wamesema hali hiyo imepelekea kutofanya kazi zao kwa ufanisi unatakiwa. Aidha, wameiomba serikali kuwasaidia walimu wenye ulemavu kwa kupunguza changamoto zinazowakabili ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa

Walimu wenye ulemavu wamesema wamekuwa wakikaliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo miundombinu kutokuwa rafiki kwao.

Wakizungumza leo jijini Dodoma katika kongangano lililowakutanisha walimu wenye ulemavu Tanzania, wamesema hali hiyo imepelekea kutofanya kazi zao kwa ufanisi unatakiwa.

Aidha, wameiomba serikali kuwasaidia walimu wenye ulemavu kwa kupunguza changamoto zinazowakabili ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa katika majukumu yao.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo Job Ndugai ,amesema wataendelea kuikumbusha serikali kuwa katika kila majengo mapya yanayojengwa iwe ya shule, ofisi kuzingatia miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.

Kwa upande wa katibu Mkuu wa chama cha Walimu Tanzania, Mwalimu Deus Seif amezungumzia upandaji vyeo wa walimu ambapo zaidi ya walimu laki moja wamepandishwa vyeo huku akibanisha changamoto iliyopo

Na Barnabas Kisengi, Dodoma.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »