SERIKALI imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa gesi wanaouza na kupandisha bei gesi kiholela na kuwaumiza wananchi Waziri wa nishati Medard Kaleman ametoa onyo hilo jijini Dodoma mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati ikiwemo kituo cha Mtambo wa kufua na kupozea umeme kilichopo Zuzu pamoja naku kuwatembelea wasambazaji na wauzaji
SERIKALI imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa gesi wanaouza na kupandisha bei gesi kiholela na kuwaumiza wananchi
Waziri wa nishati Medard Kaleman ametoa onyo hilo jijini Dodoma mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati ikiwemo kituo cha Mtambo wa kufua na kupozea umeme kilichopo Zuzu pamoja naku kuwatembelea wasambazaji na wauzaji wa gesi.
Waziri kaleman amesema ni lazima tamko la serikali lizingatiwe ambapo mtungi wa gesi wenye kilo 6 unatakiwa kuuzwa chini ya Tsh.elfu ishirini na mbili[22,000] na mtungi wa kilo 15 inatakiwa kuuzwa chini ya elfu hamsini na tatu[53,000]
Hivyo.Waziri Kaleman ametoa maelekezo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na. Maji (EWURA] kuendelea kufanya mtazamo zaidi ili bei za gesi kushuka zaidi badala ya kupanda
Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko ya wananchi kuongezeka kutokana na bidhaa hiyo muhimu ya nishati kuanza kupanda kila kukicha hali iliyopelekea wananchi kuanza kutoa malalamiko ambapo pia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na. Maji (EWURA] imeshatoa maelekezo juu ya bei elekezi ya gesi.
Na Barnabas Kisengi, Dodoma
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *