MKE WA RAIS MWINYI AIOMBA BENKI YA CRDB KUSAIDIA UBORESHAJI MAZINGIRA KUSOMA NA KUFUNDISHIA

MKE WA RAIS MWINYI AIOMBA BENKI YA CRDB KUSAIDIA UBORESHAJI MAZINGIRA KUSOMA NA KUFUNDISHIA

MKE wa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Maryam Hussein Mwinyi ameiomba Benki ya CRDB kusaidia uboreshaji wa mazingira ya skuli za Mkoa Kusini Unguja pamoja na kuzipatia vifaa mbali mbali, ikiwemo vya Maabara ya Sayansi na vitabu  ili kuchochea maendeleo  ya kielimu  Mkoani humo. Mama Maryam ametoa ombi hilo leo wakati

MKE wa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Maryam Hussein Mwinyi ameiomba Benki ya CRDB kusaidia uboreshaji wa mazingira ya skuli za Mkoa Kusini Unguja pamoja na kuzipatia vifaa mbali mbali, ikiwemo vya Maabara ya Sayansi na vitabu  ili kuchochea maendeleo  ya kielimu  Mkoani humo.

Mama Maryam ametoa ombi hilo leo wakati alipozindua Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2021) linaloendelea katika shehiya  Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema elimu ni njia muhimu katika kuleta mabadiliko chanya, katika kufikia maendeleo ya kijamii, hivyo akatumia fursa hiyo kuipongeza Benki ya CRDB, kwa kusaidia  ujenzi wa miundombinu ya kielimu pamoja na ile ya kijamii,  sambamba na kutoa elimu kwa wajasiriamali wa Mkoa huo.

Aidha, Mama Maryam aliwataka wazazi kusimamia vyema maendeleo ya elimu ya watoto wao, kuwafunza maadili mema pamoja na kuwatunza.

Nae, Mkurugenzi Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa alisema  CRDB imeshiriki kikamilifu katika ufadhili wa miradi mbali mbali ya Maendeleo,  kutoa semina na kuandaa michezo mbali mbali katika Tamasha hilo ili kufanikisha dhamira ya Serikali ya kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa uchumi.

Alisema CRDB imewawezesha wananchi kadhaa kwa kuwapatia mitaji, pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo mbali mbali kwa ajili  Tamasha hilo, kwa dhamira ya  kuibua na kuendeleza vipaji viliopo, huku ikitenga kiasi cha  shilingi Milioni  20 kwa ajili ya zawadi.

Mapema, Katibu wa Kamati ya Tamasha la Kizimkazi 2021, Hamid Abdulhamid alisema Tamsha hilo linalofanyika kila mwaka mwaka limekuwa kichocheo katika kuimarisha  shughui mbali mbali za kijamii na kiuchumi, sambamba na kuondoa changamoto mbali mbali zinazikabili jamii ya eneo hilo.

Tamasha la Kizimkazi 2021 (Kizimkazi Festival 2021) lilianzishwa rasmi mwaka 2016 likitambulika kwa jina la Samia Day, kabla kubadilishwa jina mwaka 2018 na kuitwa Kizimkazi Day, likizishirikisha shehiya tatu za Kizimkazi Mkunguni, Kizimkazi Dimbani pamoja na Kibuteni, ambapo limepata mafanikio mkubwa katika uimarishaji wa huduma na miundombinu ya kijamii.

Kwa mwaka huu  wa 2021 Benki ya CRDB ndio mfadhili mkuu wa Tamasha hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »