MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ASHIRIKI IBADA YA KUMUAGA PADRE HAULE

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ASHIRIKI IBADA YA KUMUAGA PADRE HAULE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Mbonimpawe Mpango wameshiriki ibada ya kumuaga marehemu Padre Paul Haule aliyekuwa Paroko Msaidizi wa  Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay Jijini Dar es salaam. Marehemu Padre Paul Haule pia alikuwa  Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari vya Tumaini vinavyomilikiwa na Kanisa katoliki hapa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Paroko Msadizi wa Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay – Dar es salaam marehemu  Padre Paul Haule mara alipofika kanisani hapo kushiriki ibada ya kumuaga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akitoa salamu za rambirambi za serikali kwa waombolezaji waliojitokeza katika ibada ya kumuaga marehemu Padre Paul Haule iliofanyika katika kanisa katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Mbonimpawe Mpango wameshiriki ibada ya kumuaga marehemu Padre Paul Haule aliyekuwa Paroko Msaidizi wa  Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay Jijini Dar es salaam. Marehemu Padre Paul Haule pia alikuwa  Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari vya Tumaini vinavyomilikiwa na Kanisa katoliki hapa nchini.

 Mara baada ya ibada ya kumuaga Padri Haule, Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amemtaja marehemu padre Haule kuwa mtu aliependa kuhubiri Amani na wakati wote alikua mpole na mnyenyekevu.

Amesema Kanisa limempoteza padre aliyekuwa mvumilivu wakati wote na amewaomba waumini kuendelea kumuombea marehemu Padre Haule ili apumzike kwa amani.

 Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona. Aidha amewaasa waumini kuendelea kuwakinga viongozi wa dini dhidi ya ugonjwa huo hasa katika wakati wanapokutana kupokea huduma kutoka kwa viongozi hao. Amesisitiza Viongozi wa dini pamoja na waumini kuvaa barakoa wakati wote wanapokuwa katika ibada na katika maombezi mbalimbali yanayofanyika hususani kwa wagonjwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »