UVCCM KUANZISHA LIGI YA VIJANA “UVCCM Premier Cup”

UVCCM KUANZISHA LIGI YA VIJANA “UVCCM Premier  Cup”

Na Barnabas Kisengi, Dodoma JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) inatarajia kuanzisha Ligi ya Vijana itakayoitwa  UVCCM Premier Cupambayo itajumuisha vijana wa Nchi nzima lengo likiwa ni kuibuka na kuviendeleza  vipaji vilivyopo katika maeneo hayo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo  Agosti 24,2021 jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenan Kihongosi

Na Barnabas Kisengi, Dodoma

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) inatarajia kuanzisha Ligi ya Vijana itakayoitwa  UVCCM Premier Cupambayo itajumuisha vijana wa Nchi nzima lengo likiwa ni kuibuka na kuviendeleza  vipaji vilivyopo katika maeneo hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo  Agosti 24,2021 jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenan Kihongosi amesema ligi hiyo itaitwa UVCCM Premier Cup ambayo itachezwa Tanzania Bara na visiwani lengo likiwa ni kuendeleza vipaji ambavyo vipo katika maeneo hayo.

“Kama umoja wa Vijana tumeanzisha Ligi ya Mpira ya vijana itaitwa UVCCM Premier Cup na itachazwa Tanzania nzima Bara na Visiwani,tunaenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ukisoma kifungu cha tatu sura  ya 81 kinaelezea masuala ya michezo

“Sote tunatambua michezo ni ajira na fursa na katika michezo kuna wasanii wakubwa kina Diamond Platnumz na Ally Kiba wanaitangaza Nchi yetu kwa kupitia Sanaa tunawachezaji kina Mbwana Samatta wameweza kupata  kipato,”amesema kihongosi

Kihongosi Amesema anaamini kupitia ligi hiyo wataweza kuibua vipaji na kufungua fursa za vijana mbalimbali wenye vipaji ambao hawakuweza kuonekana.

“Tunaamini Ligi hii itaenda kufungua fursa za vipaji vya Tanzania na sisi Umoja wa Vijana wa CCM tunataka kuwaambia watanzania tunagusa kila ‘angle’ na kila sehemu kwamba vijana wenye vipaji tutawashirikisha na kufungua fursa zao vijana wa ngoma na maigizo na Netbalii na vipaji tutaviendeleza,” amesema.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »