WAZIRI AWESO AFANYA UTEUZI MKURUGENZI DUWASA-JIJINI DODOMA

WAZIRI AWESO AFANYA UTEUZI MKURUGENZI DUWASA-JIJINI DODOMA

Na Barnabas Kisengi, Dodoma  Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awaso kwa mamlaka aliyonayo kwa kifungu namba 17 (1) cha sheria namba 5 ya usimamizi wa maji na idadi wa mazingira ya mwaka 2019 amemteuwa Mhandisi ARON JOSEPH kuwa Mkurugenzi Mtendaji WA Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (Duwasa) kuanzia sasa.  Uteuzi

Na Barnabas Kisengi, Dodoma 


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awaso kwa mamlaka aliyonayo kwa kifungu namba 17 (1) cha sheria namba 5 ya usimamizi wa maji na idadi wa mazingira ya mwaka 2019 amemteuwa Mhandisi ARON JOSEPH kuwa Mkurugenzi Mtendaji WA Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (Duwasa) kuanzia sasa. 


Uteuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Bodi Prof FAUSTINE BEE wakati wa kikao cha 37 cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika Agosti 3 2021 jijini Dodoma katika Ofisi kuu ya Duwasa
Bodi ya Duwasa inampongeza Mhandisi ARON JOSEPH kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa na kumuhakikishia Mkurugenzi hiyo kumpatia ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuwahudumia wananchi na wakazi wa Jiji la Dodoma na wilaya ya Bahi,Kongwa na Chamwino pamoja na mamlaka za maji zinazosimamiwa na Duwasa  za miji ya Kibagwa na Mpwapwa ili kuhakikisha wanatekeleza shading ya serikali ya kumtua mama ndio kichwani. 


Mhandisi ARON JOSEPH awali Alikuwa kaimu MkuRugenzi Mtendaji wa mamlaka ya maji Moshi kabla ya kuhamishiwa jijini Dodoma na kuendelea kuwa kaimu MkuRugenzi tangu Disemba 11, 2021 hadi alipoteuliwa kuwa MkuRugenzi Mtendaji kamili wa mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira jijini Dodoma (Duwasa)  alipothibitishwa Agosti 23 2021.


Kwa upande wake MkuRugenzi Mtendaji wa Duwasa Mhandisi ARON JOSEPH amemshukuru Waziri na bodi kwa kumteua kutumikia nafasi hiyo na amewataka watumishi wa Duwasa kumpatia ushirikiano katika majukumu yake ya kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani na kuwakikisha huduma ya maji Safi na salama yanawafikia wananchi na wakazi wa Dodoma kwa kuangalia ukubwa na sasa Dodoma ndio makao makuu ya serikali hiyo ni lazima kujipanga katika utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la wananchi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »