WAZIRI PROF. MKENDA: SITATOA VIBALI UAGIZAJI SUKARI NCHINI ILI KUVISAIDIA VIWANDA VYA NDANI

WAZIRI PROF. MKENDA: SITATOA VIBALI UAGIZAJI SUKARI NCHINI ILI KUVISAIDIA VIWANDA VYA NDANI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  WAZIRI wa Kilimo,Profesa Adolf Mkenda amesema katu hatotoa kibali cha uagizaji  wa sukari nchini kwa mtu yeyote lengo likiwa ni kuvisaidia viwanda vya ndani viweze kuzalisha sukari kwa wingi. Akizungumza Agosti 30,2021,wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sense ya kilimo,mifugo na uvuvi ya mwaka 2019-2020 ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

WAZIRI wa Kilimo,Profesa Adolf Mkenda amesema katu hatotoa kibali cha uagizaji  wa sukari nchini kwa mtu yeyote lengo likiwa ni kuvisaidia viwanda vya ndani viweze kuzalisha sukari kwa wingi.

Akizungumza Agosti 30,2021,wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sense ya kilimo,mifugo na uvuvi ya mwaka 2019-2020 ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Waziri Mkenda amesema suala la uingizaji wa sukari nchini limejaa rushwa ambapo amedai kuwa ni kama madawa ya kulevya kwani imekuwa ikiwanufaisha watu wachache.

Aidha,Waziri Mkenda amesema iwapo sheria ya uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi itabadilishwa atakuwa tayari kujiuzulu kwani itakuwa imewabeba watu wenye fedha huku akisema kuwa Wizara imeweka mikakati ya kuhakikisha mbegu ya zao la Alizeti inapatikana kwa wingi.

uzinduzi wa matokeo ya sense ya kilimo,mifugo na uvuvi ya mwaka 2019-2020,Waziri Mkenda amesema sense hiyo imewasaidia kufanya uchambuzi namna ya kufanya kilimo na ufugaji bora ambapo ameeleza kuwa sekta ya mazao inachangia asilimia 15 ya pato la Taifa.

Kwa upande wake,Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Dkt.Albina Chuwa amesema lengo la sense hiyo ni kutoa taarifa  katika uzalishaji wa mazao,idadi ya mifugo na ufugaji wa samaki  ambapo amesema kuwa Tanzania itafanya sense mwakani mwezi agost 2022 ambayo itaenda kutoa majibu sahihi katika sekta ya kilimo.

Naye,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri ameiomba Wizara ya Kilimo kufungua duka la mbegu ambalo litawasaidia wakulima kuweza kununua mbegu bora kwani wengi wamekuwa wakiuziwa mbegu feki.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »