AUAWA KWA KUCHINJWA SHINGO KILIMANJARO

AUAWA KWA KUCHINJWA SHINGO KILIMANJARO

Elice Matafu, Mkazi wa Kijiji cha Mrimbo Uuo, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi ameuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana nyumbani kwake. Mwanamke huyo ameuawa usiku wa saa 2  akiwa nyumbani kwake. Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo na amesema mauaji hayo yanaviashiria vya visasi ambapo tayari


Elice Matafu, Mkazi wa Kijiji cha Mrimbo Uuo, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi ameuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Mwanamke huyo ameuawa usiku wa saa 2  akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo na amesema mauaji hayo yanaviashiria vya visasi ambapo tayari anashikiliwa kijana mmoja kwa mahojiano zaidi.

“Ni kweli huyu mwanamke ameuliwa nyumbani kwake usiku kwa kukatwa shingo na inaonekana kuna viashiria vya visasi, tayari tunamshikilia kijana mmoja kwa mahojiano zaidi,”amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini hasa chanzo cha mauaji hayo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »