VYETI VYA CHANJO YA CORONA KUTOLEWA KIELEKTRONIKI

VYETI VYA CHANJO YA CORONA KUTOLEWA KIELEKTRONIKI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema inaendelea kuboresha suala la upatikanaji wa vyeti vya chnjo ya UVIKO-19 kwa njia ya TEHAMA Kwa wananchi ambao wanauhitaji wa vyeti vya kielektroniki ambapo hadi sasa imewapatia mafunzo watoa huduma zaidi ya 1994 kutoka kwenye vituo vinavyotoa chanjo. Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini

Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema inaendelea kuboresha suala la upatikanaji wa vyeti vya chnjo ya UVIKO-19 kwa njia ya TEHAMA Kwa wananchi ambao wanauhitaji wa vyeti vya kielektroniki ambapo hadi sasa imewapatia mafunzo watoa huduma zaidi ya 1994 kutoka kwenye vituo vinavyotoa chanjo.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dodoma Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi wakati akitoa ufafanuzi wa upatikanaji wa vyeti vya kielektroniki kwa watu waliochanja.

Aidha, Dkt. Subi ametoa ufafanuzi Kwa wananchi wa Dare es salaam waliochanja eneo la ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Julius na maeneo mengine maalumu siku ya uzinduzi.

 Dkt. Subi amewahimiza wananchi kupata chanjo ikiwa ni Kinga ya  UVIKO-19 kwani nisalama, zinaufanisi na ubora uliothibitishwa na shirika la afya Duniani na kuwaomba wananchi waendelee kuzingatia afua zote za Kinga ikiwemo kunawa mikono Kwa maji safi na sabuni kuvaaa barakoa na kutumia vitakasa mikono.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »