HALMASHAURI YA MPWAPWA YATENGA MILIONI 100 KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA ELIMU

HALMASHAURI YA MPWAPWA YATENGA MILIONI 100 KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA ELIMU

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa  Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa imetenga kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kutoka kwenye makusanyo ya mapato ya ndani na kuzielekeza fedha hizo kwenda kutatua changamoto katika sekta ya elimu wilayani hapo.  Kauli imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi Ally wakati akizungumzia vipaombele vya kazi za miradi ya maendeleo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi Ally
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa 


Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa imetenga kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kutoka kwenye makusanyo ya mapato ya ndani na kuzielekeza fedha hizo kwenda kutatua changamoto katika sekta ya elimu wilayani hapo. 


Kauli imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi Ally wakati akizungumzia vipaombele vya kazi za miradi ya maendeleo katika Halimashauri wakati wa kikao cha baraza la madiwani la Halimashauri hiyo. 
“Tumetenga  kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitakwenda kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Kama kumalizia baadhi ya maboma, madawatu na ujenzi wa vyoo tunaanza na hizo fedha na tutaendelea kutenga fedha kwa kutumia mapato yetu ya ndani ili kuhakikisha tunapunguza kidogokidogo changamoto za sekta ya elimu kwa kuanzia sasa”alisisitiza Mwanahamisi.


Aidha MWANAHAMISI amesema halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ina jumla ya Kata 33 na inamajimbo mawili Jimbo la Mpwapwa mjini na Jimbo la Kibakwe hivyo bado kuna changamoto katika sekta ya elimu kama uchakavu wa vyumba vya madarasa, umaliziaji wa maboma yaliyoanzishwa na wananchi.


George Fuime ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa amewataka waheshimiwa Madiwani kuhakikisha katika vikao vyao vya maendeleo katika Kata zao wahakikishe wanajiwekea vipao mbele vya miradi ambayo inagusa moja kwa moja Hanoi. 


Aidha FUIME amesema atahakikisha fedha hizo ambazo zitapelekwa kwenda kuboresha sekta ya elimu wanazisimamia vizuri ili zilete matokeo mazuri kwa kuwa na mapato yao ya ndani hivyo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa kuboresha elimu wilayani hapa. 
Mwenyekiti Fuime akatoa msisitizo kwa wanchi wa wilaya ya mpwapwa kuhakikisha wanakuwa wanajitokeza katika shughuli za maendeleo zinatolewa na serikali katika Kata zao huku akiwaimiza madiwani kuhakikisha wanasimamia shughuli za maendeleo katka Kata na kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya ugonjwa wa uviko 19 kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali na kuhakikisha mashuleni kunakuwa na vifaa vyote vya kujikinga na ugonjwa huo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »