WAZIRI GWAJIMA ASEMA CHANJO YA CORONA KUANZA KUTOLEWA NJE YA VITUO VYA AFYA

WAZIRI GWAJIMA ASEMA CHANJO YA CORONA KUANZA KUTOLEWA NJE YA VITUO VYA AFYA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amesema kuwa chanjo ya UVIKO-19 itaanza kutolewa maeneo yasiyokuwa na vituo vya kutolea huduma za afya kupitia huduma ya mkoba ili kufikisha huduma hiyo kwa watu wote wanaohitaji.  Dkt. Gwajima amesema hayo wakati alipohudhuria mechi ya kirafiki

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amesema kuwa chanjo ya UVIKO-19 itaanza kutolewa maeneo yasiyokuwa na vituo vya kutolea huduma za afya kupitia huduma ya mkoba ili kufikisha huduma hiyo kwa watu wote wanaohitaji. 


Dkt. Gwajima amesema hayo wakati alipohudhuria mechi ya kirafiki iliyoandaliwa kwa ajili ya uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO-19 kati ya timu viongozi wa dini mbalimbali wanaounda kamati ya amani na timu ya wachambuzi wa habari za michezo, iliyofanyika tarehe 02/09/2021 katika uwanja wa Chamanzi Complex jijini Dar ea Salaam. Dkt. Gwajima amesema kuwa kutokana na elimu inayoendelea kutolewa imesaidia kuongeza uelewa kwa watu na kuongeza mahitaji ya chanjo hasa kwa watu wanaoishi maeneo yasiyokuwa na vituo vya kutolea huduma za afya kwani wizara imekuwa ikipokea simu nyingi kutoka kwa watu hao wakihoji juu ya upatikanaji wa chanjo za UVIKO-19 katika maeneo yao, na hivyo njia ya mkoba itakuwa ni njia mbadala ya kuwafikia watu wengi zaidi. “Watu wengi sasa wameelimika baada ya kuona Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan amechanja, Mhe. Waziri Mkuu naye amechanja, majeshi yetu yamechanja wamepata amani na kupitia watu waliochanja na kuona wanaendelea vizuri, mashaka yao yanaendelea kupungua na kuulizia chanjo hizo” Amesema Dkt. Gwajima. 

Aidha,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa Wizara ya habari itaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19 kwa kupitia wasanii, wanamichezo na wanahabari. “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa viongozi wetu wa dini pamoja na wanahabari kwa kutumia mechi hii ya kirafiki kama sehemu ya kampeni ya kuendelea kutoa wito kwa watanzania kutilia maanani elimu na kampeni zinazoendelea kutolewa za utoaji wa chanjo ya UVIKO-19” amesema Mhe. Bashungwa. 

Naye Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekhe Abubakar Zubeir amesema kuwa ni muhimu watu kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara kwa sabani na maji yanayotiririka au kutumia vipukusi pamoja na kupata chanjo ya UVIKO 19. “Pamoja na Serikali kutuambia kuwa kuchanja ni hiari mimi napenda kutoa rai kwa vijana na watu wazima kuchagua kuchanja kwani inafaida kubwa kuliko kutokuchanja kama tunavyoelekezwa na wataalamu kwamba kwa mtu aliyechanja anakuwa salama zaidi hata kama atapata maambukizi ya ugonjwa huu madhara hayawezi kuwa makubwa ukilinganisha kwa mtu asiyepata chanjo. Pia kwa sisi waislamu chanjo itatusaidia sana hata katika kutekeleza ibada zetu hususani kufanya hija na umra inayotekelezwa huko Saudia Arabia, kwani hivi sasa huwezi kuingia katika nchi hiyo bila ya kupata chanjo” amesema Shekhe Zubeir.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »