BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA BUNGE

BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA BUNGE

Na Barnabas Kisengi, Dodoma   BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo mbalimbali kwa timu ya Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bunge sport club) vyenye thamani ya shilling million 12 kwa ajili ya tamasha litakalofanyika septemba 2 mwaka huu kati ya timu ya bunge na timu ya NMB katika uwanja wa jamhuri na viwanja vya

Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abass Tarimba (katikati) kwa ajili ya Tamasha la NMB na wabunge litalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma. Kushoto ni Mwakamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club Mhe. Esther Matiko
Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abass Tarimba (katikati) na Makamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club Mhe. Esther Matiko wakionyesha jezi zitakazotumika kwenye ya Tamasha la NMB na Wabunge litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.
Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abass Tarimba (katikati) na Makamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club Mhe. Esther Matiko wakionyesha mipira itakayotumika kwenye ya Tamasha la NMB na Wabunge litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma

Na Barnabas Kisengi, Dodoma 

 BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo mbalimbali kwa timu ya Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bunge sport club) vyenye thamani ya shilling million 12 kwa ajili ya tamasha litakalofanyika septemba 2 mwaka huu kati ya timu ya bunge na timu ya NMB katika uwanja wa jamhuri na viwanja vya chinangali park.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi viifaa hivyo katika ukumbi wa HABARI Bungeni jijini DODOMA, afisa mkuu wa fedha wa NMB Juma Kimori Amesema kuwa michezo itakayohusishwa ni pamoja na mpira miguu,Basketball wanaume na wanawake,mpira wa wavu,netball,kuvuta kamba na kukimbiza kuku.

Aidha,kimori ameeleza kwamba wao kama NMB wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa jamiii inapenda michezo kwani michezo ni Muhimu kwa afya,mahusiano mazuri baina ya jamii na serikali huku akisema nmb inatambua mchango mkubwa wa bunge katika kutunga sheria mbalimbali pamoja na wajibu wa kusimamia serikali ndani na nje ya Bunge.

Akizungumza kwa niaba ya  wabunge mwenyekiti wa Bunge sport club Tarimba Abbas ameishukuru NMB kwa mchango wao wa kutoa vifaa vya michezo kwa timu ya bunge sport club ambapo amesema kuwa itakuwa chachu kubwa ya kujenga umoja na mahusiano mazuri huku akiomba uongozi wa timu ya NMB kutotafuta wachezaji ambao siyo wafanyakazi wa NMB ili mchezo uchezwe kwa Haki.

Sambamba na hayo timu ya nmb na bunge sport club zinatarajia kufanya tamasha hilo siku ya jumamosi septemba 4 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri na viwanja vya chinangali park huku tamasha hilo likibeba kauli mbiu ya ‘”kivumbi na jasho”.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »