UNWTO KUWEKA MIKAKATI YA KWAJENGEA UWEZO WADAU WA UTALII NCHINI TANZANIA

UNWTO KUWEKA MIKAKATI YA KWAJENGEA UWEZO WADAU WA UTALII NCHINI TANZANIA

NA MWANDISHI WETU MAALUM KISIWA CHA SAL-CAPE VERDE Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masula ya  Utalii Duniani  ( UNWTO) limeahidi kushirikiana na Tanzania katika kuweka mikakati bora ya kuwajengea uwezo  watu waliopo katika sekta ya utalii nchini kuanzia mwezi juni 2022 Hatua hiyo inakuja kufuatia hali mbaya ya ugonjwa wa COVID  kuidhoofisha sekta ya utalii

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi mbalimbali  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  tarehe 2 Septemba  hadi 6 mwaka huu  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo akiwa pamoja na maofisa wa utalii waliombatana na ujube kutoka Tanzania
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa pili  kushoto) akimkabidhi  moja ya zawadi yenye nembo ya Mlima Kilimanjaro   Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  tarehe 2 Septemba  hadi 6 mwaka huu  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akifanya kikao cha ana kwa ana na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika hilo la Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  tarehe 2 Septemba  hadi 6 mwaka huu  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO), Zurab Pololikashvili mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana ambapo UNWTO limeahidi kushirikiana na Tanzania katika kuweka mikakati bora ya kuwajengea uwezo  watu waliopo katika sekta ya utalii nchini kuanzia mwezi juni 2022
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa pili  kushoto) akimuonesha  baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo katika jarida la Utalii kutoka Tanzania Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  tarehe 2 Septemba  hadi 6 mwaka huu  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa pili  kushoto) akimkabidhi  moja ya zawadi ya kopo la kahawa yenye  nembo ya Mlima Kilimanjaro   Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  tarehe 2 Septemba  hadi 6 mwaka huu  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde

NA MWANDISHI WETU MAALUM KISIWA CHA SAL-CAPE VERDE

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masula ya  Utalii Duniani  ( UNWTO) limeahidi kushirikiana na Tanzania katika kuweka mikakati bora ya kuwajengea uwezo  watu waliopo katika sekta ya utalii nchini kuanzia mwezi juni 2022

Hatua hiyo inakuja kufuatia hali mbaya ya ugonjwa wa COVID  kuidhoofisha sekta ya utalii nchini na Duniani kwa ujumla huku  Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC) ikikadiriwa kupata hasara ya dola 4.8 bilioni za Marekani ( zaidi ya Sh. trioni 11) kwenye sekta ya utalii kutokana na janga la  Corona huku watu milioni 21 wakikosa ajira

Akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro katika kikao cha pembeni mwa mkutano wa UNWTO  wa 64 wa Kanda ya Africa ukilenga kufungua fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii hasa katika kipindi ambacho sekta ya utalii inachechemea kutokana na kushambuliwa na ugonjwa wa Corona    Katibu Mkuu wa UNWTO Zurab Pololiskashvil  amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa Wadau wa Utalii na ili waweze kuendana na janga la Corona katika kuendesha shughuli za utalii nchini

Mkutano huo wa UNWTO wa 64 wa Kanda ya Afrika unafanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde ambapo umewakutanisha mawaziri 30 wa utalii Barani Afrika ukilenga kujadili mustakabali wa utalii barani Afrika na Duniani kwa ujumla kufuatia uwepo wa janga la ugonjwa wa Corona

 Kat Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo  unaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  akiwa na maofisa na Makamishna Uhifadhi kutoka TFS na TAWA, maofisa pamoja na Balozi wa Tanzani nchini Ufaransa Mhe, Samuel Shelukindo.

Aidha, Katika kikao hicho Katibu Mkuu amesema  mafunzo hayo yatazilenga jamii zinazozunguka vivutio vya utalii ili kuzijengea uwezo wa kushiriki moja kwa moja katika shughuli za  utalii nchini likiwa lengo ni kutengeneza ajira nyingi zaidi kupitia sekta hiyo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo amemueleza Waziri Dkt.Ndumbaro kuwa UNWTO  iko mbioni kuandaa kalenda  ya mwaka ya UNWTO  ambapo Tanzania nayo itakuwepo ktk orodha hiyo ya  kuendana na matukio yatakavyopangwa katika mkutano huo

Amesema moja ya kipaumbele cha UNWTO kwa sasa ni kuitangaza Tanzania na Africa kwa ujumla

Akizungumza katika kikao hicho cha ana kwa ana na Katibu Mkuu huyo, Dkt.Ndumbaro amesema mafunzo hayo yatatoa matumaini kwa Wadau wa Utalii nchini baada ya ugonjwa wa Corona kuwatikisa

Hata hivyo, Dkt.Ndumbaro amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwa kufanya vizuri katika  shughuli za Uhifadhi lakini  katika suala la kujitangaza na kutafuta masoko ya utalii imekiwa haifanyi vizuri hivyo ujio wa mafunzo hayo yataiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika nyanja hiyo.

Aidha, Dkt.Ndumbaro amemualika Katibu Mkuu wa UNWTO,  Zurabu Pololikashvil kuja kutembelea vivutio volivyopo Tz na kusisitiza kuwa ataambatana naye katika ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »