Silaa, Polepole, Gwajima wahojiwa na kamati maadili ya wabunge CCM

Silaa, Polepole, Gwajima wahojiwa na kamati maadili ya wabunge CCM

Na Barnabas Kisengi ,Dodoma  KAMATI ya maadili ya  Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) imekamilisha zoezi la kuwahoji  Wabunge wa chama hicho akiwemo Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Jimbo la Kawe Dar-es-salaam, Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar-es-salam Jerry Silaa na aliyekuwa katibu wa NEC Itifaki na uenezi Humphrey Polepole ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa. Akizungumza na

Na Barnabas Kisengi ,Dodoma 

KAMATI ya maadili ya  Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) imekamilisha zoezi la kuwahoji  Wabunge wa chama hicho akiwemo Askofu Josephat Gwajima Mbunge wa Jimbo la Kawe Dar-es-salaam, Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar-es-salam Jerry Silaa na aliyekuwa katibu wa NEC Itifaki na uenezi Humphrey Polepole ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Doddoma katika ofisi cha chama hicho mara baada ya kamati ya maadili kumaliza zoezi la kuwahoji wabunge hao Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya wabunge wa chama cha mapinduzi (CCM) Hassan Mtenga ameeleza kuwa yale ambayo wameyapata kupitia mahojiano hayo watayapeleka jumatatu Septemba 6 Mwaka huu  kwenye kamati ya uongozi wa bunge ambaye mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa bunge ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kassim majaliwa  ili yafanyiwe maamuzi.

Kwa upande wake Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa Habari amesema yeye sio mzungumzaji bali kamati hiyo ndio itazungumza.

Ikumbukwe kuwa wabunge hao walifikishwa kwenye Kamati  ya maadili haki na madaraka ya Bunge ambapo mbunge wa kawe askofu josephat gwajima alihojiwa tarehe 23 mwezi wa 8 na mbunge wa jimbo la ukonga jerry silaa tarehe 24 mwez wa 8 mwaka huu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »