ZAIDI YA TSH MILIONI 72.2 ZAPATIKANA KWA AJILI YA UJENZI WA MADHABAHU.

ZAIDI YA TSH MILIONI 72.2 ZAPATIKANA KWA AJILI YA UJENZI WA MADHABAHU.

Na Emesto Eliudy, Dar Es Salaam. Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata-Liwiti, limekusanya kiasi Cha zaidi ya Tsh. Milioni 72. 2 kwa lengo la kujenga Madhabahu na Miundombinu mbalimbali ya Kanisa Hilo ikiwemo ukarabati wa nyumba ya Mchungaji. Akizungumza jijini Dar ES Salaam, Mchungaji wa Kanisa Hilo, Mch. Emmanuel Mahemb alisema

Na Emesto Eliudy, Dar Es Salaam.


Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata-Liwiti, limekusanya kiasi Cha zaidi ya Tsh. Milioni 72. 2 kwa lengo la kujenga Madhabahu na Miundombinu mbalimbali ya Kanisa Hilo ikiwemo ukarabati wa nyumba ya Mchungaji.

Mchungaji Wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata-Liwiti, Mch. Emmanuel Mahembo.


Akizungumza jijini Dar ES Salaam, Mchungaji wa Kanisa Hilo, Mch. Emmanuel Mahemb

alisema kuwa lengo la kukusanya fedha hizo ni kuboresha Muonekano wa Madhabahu, ununuzi wa Mabenchi pamoja na Ukarabati wa Nyumba ya Mchungaji.


“Changizo Hilo limebeba Makusudio makuu matatu, ikiwemo kuboresha Muonekano wa Madhabahu, ununuzi wa Mabenchi ya kukalia ili tuondokane na Viti vya Plastiki na kukarabati Nyumba ya Mchungaji ambayo ilionekana haijakamilika baada ya Ujenzi wa awali”. Alisema Mch. Mahembo

Aidha Mch. Mahembo aliongeza kuwa kufanyika kwa Changizo Hilo ni kupandisha hadhi ya Mungu wanaemtukia Kwani Muonekano wa Sasa wa Kanisa Hilo hauendani na Hadhi ya Mungu wanae mtumikia.

“Lengo Kubwa ni kupandisha hadhi ya Mungu wetu tunaemtumikia, Mungu wetu sisi siyo mnyonge kiasi hicho. Namna ambavyo tunaonekana na namna ya Mazingira tuliyonayo au Muonekano wa Madhabahu yake jinsi ulivyo hauendani na kiwango Cha Mungu tunaemtumikia” alisema Mch. Mahembo.

“Tunataka Sasa hadhi ya Mungu tunaemtumikia iendane na Madhabahu yake jinsi ilivyo na haiishii tu kwenye Madhabahu Bali iendane pia hata kwenye Samani yaani viti vya Wakristo lakini pia hata Ofisi ya Mchungaji itakwenda kubadilika” aliongeza Mch. Mahembo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia alikua Mgeni katika Changizo Hilo,  Felistas Mushi alisema kuwa kujenga Madhabahu ni kuweka agano na Mungu kwani Mungu anatimiza maagano yake Kupitia Madhabahu.

Mkurugenzi Msaidizi-Katiba na Sheria, Felistas Mushi

“Kujenga Madhabahu siku zote ni kuweka agano na Mungu kwa sababu Mungu hua anaongea na ni Mungu wa maagano pia ni Mungu wa Madhabahu kwahiyo unavyomjengea Mungu Madhabahu unaweka ahadi na yeye kwa ajili yako wewe akufanyie Jambo Gani katika Maisha yako”. Alisema Mkurugenzi Huyo.

Pia Mkurugenzi Huyo aliongeza kwa kusema kuwa ni muhimu Sana kwa Wakristo kufahamu kwamba wanapoitwa Kujenga Madhabahu wanaitwa kufanya agano na Mungu.

“Ni muhimu Sana kwa Mkristo kufahamu kwamba anapoitwa kujenga Madhabahu anaitwa kwenda kufanya agano. Mungu akitaka kukubariki Siku zote anakupa Wajibu. Nawasihi Wakristo wote suala lolote ambalo ni la kumtumikia Mungu walichukulie kwa Uzito kwasababu ni suala la kuingia agano na Mungu na waone kama ni fursa ambayo wameipata kwa ajili ya kufanya agano na Mungu, siku zote Mungu hajawahi kuvunja agano lake”. Alisema Mkurugenzi huyo

Akiwasilisha risala ya kamati ya Ujenzi katika Kanisa hilo kwa Mgeni Rasmi,  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fridah Malasusa alisema kuwa lengo la kamati hiyo ni kukusanya kiasi Cha Tsh. Milioni 130 ambapo tayari wamekwisha kusanya Tsh. Milioni 18 kutoka kwa waumini na marafiki zao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata-Liwiti, Bi. Fridah Malasusa


“Ndugu Mgeni Rasmi, lengo letu ni kukusanya kiasi Cha Tsh. Milioni 130 ambazo tunatarajia kuzipata kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na michango ya waumini wa Kanisa hili.
Zoezi hili tulilianza  miezi kadhaa nyuma ambapo mpaka Sasa tumefanikiwa kukusanya kiasi Cha Tsh. Milioni 18 Taslimu kutoka kwa waumini na Marafiki zao. Hivyo siku hii ya Leo ambayo wewe ni Mgeni Rasmi tunakusudia kukusanya kiasi Cha Tsh. Milioni 113 ambayo ni pungufu ya Tsh. Milioni 130.” Alisema Fridah 


Nao baadhi ya Waumini wa Kanisa Hilo,Bw. Thomson Mwasichili na Bi. Jesca anyingisye, walisema kuwa wanategemea kuona mabadiliko makubwa katika Kanisa lao kwa kuwa na Muonekano wa kisasa kwani Ujenzi wa Madhabahu mpya utabadilisha Muonekano wa Kanisa hilo.

Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata-Liwiti wakiwa katika Harambee ya Changizo la Ujenzi wa Madhabahu.


“Tunategekea baada ya Zoezi hili kuona Ushirika wetu umekuwa Ushirika wa kisasa, ninaposema Ushirika wa kisasa Nina maana kwamba Madhabahu Sasa itakua Madhabahu mpya na itakua ya Kidigitali na tutaweza kuona ibada zetu live kwa maana Washirika tutakua na uwezo wa kupata mahubiri kila siku kwa njia ya mtandao”. Alisema Bw. Thomson Mwasichili.

Mgeni Rasmi, Felistas Mushi akikabidhi Fedha Taslimu kiasi Cha Tsh Milioni 16 kwa Mchungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata-Liwiti, Mch. Emmanuel Mahembo.

“Tulikua tunatamani siku hii ifike na tuone vile Mungu anaweza akatufikisha Mahali ambapo tulikua tunatamani kufika kwa kifupi tumebarikiwa na watu wameguswa na kuonyesha Nia ya Dhati na moyo wa unyenyekevu  wa kumtolea Mungu kwa habari ya kubadilisha Muonekano wa Madhabahu yetu ambayo tuna muabudia Mungu”. Alisema Bi Jesca.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »