JUMLA YA WANAFUNZI 6552 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU DARASA LA SABA KESHO WILAYANI MPWAPWA

JUMLA YA WANAFUNZI 6552 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU DARASA LA SABA KESHO WILAYANI MPWAPWA

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa  Jumla ya wanafunzi 6552 wa shule za msingi wilayani Mpwapwa wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la Saba inayotarajiwa kufanyika kesho hapa nchini  Akizungumza na jfivetv.com Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mwanahamisi Ally amesema maandalizi yote yamekamilika vizuri na jumla ya shule 129 zilizopo wilayani mpwapwa zinatarajiwa kufanya

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa 


Jumla ya wanafunzi 6552 wa shule za msingi wilayani Mpwapwa wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la Saba inayotarajiwa kufanyika kesho hapa nchini 

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mwanahamisi Ally


Akizungumza na jfivetv.com Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mwanahamisi Ally amesema maandalizi yote yamekamilika vizuri na jumla ya shule 129 zilizopo wilayani mpwapwa zinatarajiwa kufanya mitihani hiyo. 


Mwanahamisi Ally amesema kuwa wasimamizi wote waliopangiwa vituo vya kusimamia wamekamilika na amewataka kuhakikisha wanasimamia vizuri mitihani hiyo na wasije wakajihusisha na uvujaji.


Aidha Mkurugenzi Mwanahamisi amewashukuru walimu kwa kuweze kuhakikisha wanafunzi wamepata elimu kwa kipindi cha miaka saba na amewapongeza wanafunzi hao kwa kumaliza shule na kuwatakia mtihani mwema wanao tarajia kuanza kuufanya kesho. 


Mwanahamisi amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi hao wanao maliza kuhakikisha wanaanza kuwaanda mapema kwa ajili ya kuanza kidatu cha kwanza mwakani.


Adha amewataka watendaji wa Kata na vijiji kuhakikisha wanasimamia vizuri ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vinaendelea kujengwa wilayani hapa kwa kushirikisha na wananchi katika  katika maeneo yao ili kuhakikisha mwakani wasiwe na upungufu wa vyumba vya madarasa. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »