WIZARA YA MADINI, NHC ZASAINI MKATABA UJENZI WA OFISI DODOMA

WIZARA YA MADINI, NHC ZASAINI MKATABA UJENZI WA OFISI DODOMA

Na Mwandishi wetu Dodoma Wizara ya Madini imesaini Mkataba wa Shilingi Bilioni 22.02 na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa kuanza ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Hafla ya kusaini Mkataba wa ujenzi huo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini Mtumba jijini Dodoma Septemba 7, 2021 ambapo

Na Mwandishi wetu Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (Kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani (Kushoto) wakisaini Mkataba wa kuanza kwa ujenzi waOfisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Septemba 7, 2021jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani, akisaini Mkataba wa kuanza kwa ujenzi wa Ofisi zaWizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Septemba 7, 2021 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani, akisaini Mkataba wa kuanza kwa ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Septemba 7, 2021 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA Wenzelaus Kizaba, akizungumza baada ya kusaini Mkataba wa kuanza kwa ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Septemba 7, 2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani na wataalam wengine wakiangalia eneo la ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Septemba 7, 2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (Kulia) na Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA Wenzelaus Kizaba (Kushoto) wakisaini Mkataba wa kuanza kwa ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Septemba 7, 2021 jijini Dodoma


Wizara ya Madini imesaini Mkataba wa Shilingi Bilioni 22.02 na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa kuanza ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Hafla ya kusaini Mkataba wa ujenzi huo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini Mtumba jijini Dodoma Septemba 7, 2021 ambapo pia, Wizara imekabidhi rasmi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi NHC baada ya kushinda zabuni.


Aidha, katika hatua nyingine, wizara imesaini Mkataba na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa ajili kuwa msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Msanjila ameipongeza NHC kwa kushinda kandarasi hiyo na kutaka ujenzi uwe wa haraka kwa kuzingatia ubora, viwango na kasi kama ilivyo kwa sura ya Madini.
“Ni matumaini yangu kwamba NHC wana uzoefu mkubwa, siku za karibuni wamekamilisha miradi mikubwa ya Kitaifa, hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kusini, lakini pia hospitali ya Kanda ya Mara na majengo mengine mengi,” amesema Prof. Msanjila.


Aidha, Prof. Msanjila amesema, msimamizi wa ujenzi huo ambaye ni (Consultant) Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ndiye aliyesanifu ramani inayokwenda kutumika kujenga jengo la Wizara ya Madini.
“Kitu walichokisanifu watakuwa na mazingira mazuri ya kukisimamia wao wenyewe na hatutegemei changamoto za nenda rudi, na kwa sababu ni taasisi zote za Serikali na zimefanya kazi kwa pamoja katika miradi mingi, ninaamini wanauelewa mkubwa wa karibu na utekelezaji wa maradi huu utakuwa kwa ufanisi sana,” ameongeza Prof. Msanjila


Naye, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani amemueleza Prof. Msanjila kuwa, NHC watatekeleza mradi huo kwa ustadi mkubwa kwa kuhakikisha dhamira wizara inayo kwao katika muda ambao mradi unatakiwa kukamilika.

“Tutajitahidi kuwa ndani ya muda kwa asilimia 100, ombi langu kwa wenzetu TBA twende haraka kwa pamoja ili tufike kama kauli mbiu ya Rais inavyosema. Kwa hiyo tujitahidi kwenda haraka kwa pamoja ili tufike kwa haraka kule ambapo tunataka kwenda,” ameongeza Dkt. Banyani.


Dkt. Banyani amehaidi kutekeleza mradi huo kwa kasi na ameishukuru Serikali kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha zitakazowezesha kutekelezwa kwa mradi na akiishukuru wizara kwa kuiamini NHC. 


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA Wenzelaus Kizaba, ameshukuru Wizara ya Madini kwa kuwapatia nafasi ya kuweza kuwa wabunifu na wasanifu wa jengo la wizara. Amesema Serikali iliwapatia kusanifu majengo yote ya Mji wa Serikali kwa Wizara zote 24 pamoja na taasisi mbili.
“Sisi na NHC tumefanya kazi nyingi, wamekuwa wakandarasi sisi tumekuwa wasimamizi, na kuna sehemu nyingine sisi tumekuwa wakandarasi na wenyewe wasimamizi kwa hiyo tunajuana. Kwa mantiki hiyo tutashirikiana kwa pamoja, na kuhakikisha kwamba hili jengo linajengwa kwa viwango vilivyokusudiwa na hakutakuwa na ucheleweshwaji wa aina yoyote kwa sababu vitu vyote vimezingatiwa ndani ya ubunifu na usanifu wa jengo la wizara,” ameeleza Kizaba.


Katika makubaliano hayo yaliyosainiwa leo, Wizara ya Madini imeonyesha eneo la ujenzi litakalojengwa jengo la Wizara ya Madini na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini, NHC, TBA ili kuanza rasmi kwa ujenzi.
Kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, kutapelekea Idara na Vitengo vyote vya wizara kuhamia katika jengo hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »