Na Barnabas Kisengi,Dodoma Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto DKt Dorothy Gwajima amesema kuwa matumizi ya takwimu zenye ubora katika ngazi za chini ili kuweza kufanya maamuzi ya kisayansi bado ni changamoto katika halmashauri nchini jambo ambalo linarudisha nyuma Sekta ya Afya. Akizungumza kwenye madhimisho ya siku ya Epidemiology Duniani leo jijini Dooma katika
Na Barnabas Kisengi,Dodoma
Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto DKt Dorothy Gwajima amesema kuwa matumizi ya takwimu zenye ubora katika ngazi za chini ili kuweza kufanya maamuzi ya kisayansi bado ni changamoto katika halmashauri nchini jambo ambalo linarudisha nyuma Sekta ya Afya.
Akizungumza kwenye madhimisho ya siku ya Epidemiology Duniani leo jijini Dooma katika viwanja vya Nyerere Square waziri huyo amesema kuwa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ili kutambua mapema viashiria hatari kwa jamii lazma pawepo na takwimu zenye ubora katika ngazi ya halmahauri.
Aidha waziri Gwajima ameeleza kuwa jumla ya watumishi mia tano kumi na mbili kutoka idara ya afya ya binadamu na idara ya afya ya mifugo wamepatiwa mafunzo katika ngazi ya kozi ya awali kutoka mikoa yote 26 na halmashauri mia moja hamsini na tisa kwa kipindi cha miaka sita.
kwa upande wake Rais wa Chama cha Wataalamu wa Epidemology na maabara Tanzania Dkt. Elibariki Mwakapeje (Tanflea) amesema kuwa wao kama Tanflea ni kuhakikisha afya ya mtanzania inaimarika ili watu waweze kuwa na afya bora ili aendelee kufanya shughuli zao za kila siku.
Madhimisho haya ya siku ya Epidemiology yamefanyia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania .
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *