WAZIRI UMMY AWAONYA WALIMU WENYE MAHUSIANO NA WANAFUNZI

WAZIRI UMMY AWAONYA WALIMU WENYE MAHUSIANO NA WANAFUNZI

NA PENDO MANGALA,DODOMA. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa badhi ya walimu wa kike na kiume ambao wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwani wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria. Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa

NA PENDO MANGALA,DODOMA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa badhi ya walimu wa kike na kiume ambao wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwani wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais -Tume ya Utumishi wa Walimu tawi la Tume ya utumishi wa walimu unaojumuisha washiriki kutoka Tume Makao Makuu, Ofisi za Tume kutoka Kanda zote na Wilaya zake 139Nchini.

Amesema ni vyema suala hilo likatiliwa mkazo kwa walimu wa kike na wakiume ili wawe  waadilifu katika kazi ambayo wanaifanya ili kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanafikia ndoto zao.

Aidha amebainisha kuwa mchakato wa ajira za Walimu kwa Mwaka ujao wa Fedha utafanywa na Tume ya walimu Nchini TSC hivyo amewaagiza kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa mchakato wa ajira za walimu kwa umakini, na endapo kazi hiyo itaingia dosari wajiandae kuwajibika huku akiiagiza Tume hiyo kumpatia taarifa sahihi ya uwiano wa walimu wa shule za msingi na sekondari ili kuimaliza changamoto hiyo.



Awali akitoa taarifa za Tume hiyo,Katibu Mtendaji wa Tume ya utumishi wa walimu nchini TSC,Paulina Mkwama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Tume hiyo  ameeleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na hatua walizochukua kwa walimu waliokiuka maadili ya utumishi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »