WANAHABARI JIJINI DODOMA WANAOMBOLEZA KIFO CHA MDAU WAO WA KARIBU

WANAHABARI JIJINI DODOMA WANAOMBOLEZA KIFO CHA MDAU WAO WA KARIBU

Na Barnabas Kisengi, Dodoma  Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (Center Peres Club) kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mdau wao wa habari Sarah Hume (Mama Innocent) kilichotokea jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamin mkapa (UDOM)  jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi.  Akizungumza na jfivetv.com Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa

Na Barnabas Kisengi, Dodoma 


Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (Center Peres Club) kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mdau wao wa habari Sarah Hume (Mama Innocent) kilichotokea jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamin mkapa (UDOM)  jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi. 


Akizungumza na jfivetv.com Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma, Mussa Yusufu amesema wao kama chama wamepokea kwa masikitiko makubwa ya kifo cha mdau wao wa sekta ya habari katika mkoa wa dodoma kwani Alikuwa mtu mwenyewe ushirikiano mkubwa sana katika tasinia ya habari mkoani Dodoma 
“Nashindwa nisemaje juu ya Marehemu mama Inno kwa Sisi waandishi wa habari hasa wa hapa jijini Dodoma kama tunavyo kumbuka Alikuwa na ofisi yake ya Intanet cafe hapa mjini iliyokuwa ikijulikana kwa jina la  APTECH na waandishi wengi walikuwa wakienda kufanya kazi zao hata inapo fika usiku alikuwa akikaa kumsubiri mwandishi hadi amalize kazi yake ndio aondoke huu ni upendo wa ajabu aliokuwa nao Sarah (mama Inno) hata wakati mwengine akiwa amejaza wateja bado anaweze kumtoa mteja amwachie mwanahabari afanye kazi yake kwanza, kwakweli naishiwa na maneno ya kusema zaidi ya kusema tumwombee katika sala zetu za kila siku mwenyezi mungu ampumzishe kwa amani” Amesema Mussa Yusufu.


Nao baadhi ya Waandishi wa Habari baada ya kupokea taarifa za msiba huo waliongea na jfivetv.com akiwemo Lussy Ndalama, Happy Mtweve, Roda Simba, Renatha Msungu, Danyelle Mkate, Imakulata, Hamida Ramadhani, Ramathani Hassan, Paulo Mabeja, sarah Mosses na Brayan Mosses wamesema wao kama wanahabari wa Mkoa wa Dodoma wamepokea kwa masikitiko makubwa ya msiba huo wa mdau wa habari Sarah Hume (mama Inno) hawana cha kusema hadi sasa kwakuwa waliishi naye kama Ndugu na muda wote waliokuwa wakifanya kazi zao hawajawahi kubugudhiwa katika utendaji wa majukumu yao ya kazi hivyo kwa pamoja wanatoa pole nyingi kwa familia na mume wake wanawaombea mwenyezi mungu awape faraja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi


Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Chinyoyo Kata ya Kilimani Bi Faustine Kisengi amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwananchi wake na mwanachama wa chama cha Mapinduzi na kada mwaminifu wa mtaa wa chinyoyo “kwakweli Sarah ametutoka hatujaamii bado kwani hapa mtaani amekulia na hata mama yake bado anaishi hapa hapa ndio makazi yake  na ndio maana mnaona watu bado wanamkimbilia kumpa faraja japo Sarah alikuwa anaishi Nkuungu na mume wake lakini walikuwa wakija huku mara kwa mara kumsalimia mama yao na hakika tumempoteza mtu ambaye bado tulikuwa tunamwitaji sasa hatuna cha kusema, Mwenyezi Mungu amemoenda zaidi hivyo twapaswa kuendelea kumwombea na kuiga mazuri yake aliyoyafanya hapa duniani akiwa hai enzi za uhai wake kuna jambo la kujifunzi sisi sote, hapa naishiwa maneno ya kuongea kikubwa tuendelee kumwaombea katika sala zetu apate pumziko la milele na kuiombea familia take mumewe,mama na ndugu wote  katika kipindi hichi kigumu cha majonzi na tukae tutafakari leo ni yeye he kesho na muda huu. Tunapaswa kuishi kwa upendo na kupendana Kama maisha aliyoishi Sarah, hakika ni mfano wa kuigwa hapa duniani” alisisitiza Faustina.


Marehemu Sarah (Mama Inno) anatarajiwa kuzikwa kesho Septemba 10, 2021 hapa jijini Dodoma 

“RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA NA MWANGA WA MLELE UMEANGAZIE! SARAH APUMZIKE KWA AMANI…….. AMINA. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »