HOTUBA YA MHE.MAJALIWA WAKATI AKIHAIRISHA MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA 12 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

HOTUBA YA MHE.MAJALIWA WAKATI AKIHAIRISHA MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA 12 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mheshimiwa Spika, leo hii tunafikia tamati ya Mkutano wa Nne wa Bunge la 12 laJamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioanza kikao chake cha kwanza tarehe 31 Agosti, Hivyo, hatunabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwakutuwezesha kuhitimisha shughuli zote zilizopangwa kwenye mkutano huu tukiwa buheriwa afya. Mheshimiwa Spika, vilevile, ninakushukuru wewe binafsi kwa kumudu kuliongozavema

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.KASSIM MAJALIWA.

Mheshimiwa Spika, leo hii tunafikia tamati ya Mkutano wa Nne wa Bunge la 12 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioanza kikao chake cha kwanza tarehe 31 Agosti,

Hivyo, hatunabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa
kutuwezesha kuhitimisha shughuli zote zilizopangwa kwenye mkutano huu tukiwa buheri
wa afya.

Mheshimiwa Spika, vilevile, ninakushukuru wewe binafsi kwa kumudu kuliongoza
vema Bunge hili tukufu, ukisaidiwa na Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa
Wenyeviti wa Bunge. Aidha, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango
mizuri mliyoitoa kwa kusema na kwa maandishi wakati wa kuchangia hoja mbalimbali
zilizowasilishwa na Serikali kwenye mkutano huu.

Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge wenzangu
kuwa, Serikali kwa upande wake ipo tayari muda wote kupokea michango yenu yenye lengo
la kusaidia kuboresha utekelezaji wa mipango yake.
Salamu za Pole

Mheshimiwa Spika, niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kukupa pole
kufuatia taarifa za kuhuzunisha za kifo cha Mheshimiwa Elias John Kwandikwa aliyekuwa
Mbunge wa Ushetu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kilichotokea tarehe 2
Agosti, 2021. Aidha, natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na
wananchi wote wa Jimbo la Ushetu kwa kuondokewa na mwakilishi wao huyo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, natoa salamu za pole kwa Kamanda Simon Nyakoro
Siro, Inspekta Jenerali wa Polisi kufuatia tukio lililotokea tarehe 25 Agosti, 2021 jijini Dar es
Salaam, ambapo askari wetu wazalendo wapatao watatu na mlinzi mmoja wa kampuni
binafsi waliuawa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kiusalama. Mwenyezi Mungu azilaze
roho za marehemu mahala pema na awape uponyaji wa haraka majeruhi wa tukio hilo.
Amin!

Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwapa pole Watanzania wenzangu
waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki na wengine kupata ulemavu katika matukio
mbalimbali ikiwemo ajali za barabarani zilizogharimu maisha ya maafisa watano wa
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), waliofariki dunia tarehe 23 Agosti, 2021 wakati
wakitekeleza majukumu yao ya kikazi mkoani Songwe. Mwenyezi Mungu aziweke roho za
marehemu mahala pema peponi. Amina!
SHUGHULI ZA BUNGE
Maswali na Majibu

Mheshimiwa Spika, wakati wa mkutano huu wa 4 wa Bunge la 12, Waheshimiwa
Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya msingi 119 na maswali 263 ya nyongeza ambayo yalijibiwa na Serikali. Kadhalika, maswali 14 ya papo kwa papo yaliulizwa na
Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Waziri Mkuu.
Maazimio ya Bunge

  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, Waheshimiwa Wabunge walijadili na kupitisha
    maazimio mawili ya Bunge kama ifuatavyo: –
    Moja: Azimio la Bunge kuhusu kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya
    Viwango vya Afya ya Mimea, Wanyama na Usalama wa Chakula (East African
    Community Protocol on Sanitary and Phytosanitary – SPS Measures);

Mbili: Azimio la Bunge kuhusu kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (African Continental Free Trade Area – AfCFTA); na

  1. Mheshimiwa Spika, kuridhiwa kwa maazimio haya kutasaidia nchi yetu kuimarisha
    biashara na uwekezaji kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki sambamba na kuongeza
    shughuli za biashara na uwekezaji wa ndani baina ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
    Halikadhalika, kutaiwezesha Tanzania kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine
    wanachama wa Umoja wa Afrika.
    Miswada ya Sheria
  2. Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge pia, walijadili na kupitisha miswada
    mitano ya sheria iliyowasilishwa na Serikali katika mkutano huu kama ifuatavyo: –
    Moja: Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.2 wa Mwaka 2021;
    Mbili: Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.4 wa Mwaka 2021;
    Tatu: Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Wahasibu na

Wakaguzi wa Hesabu wa Mwaka 2021;

Nne: Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wa Mwaka 2021. Marekebisho haya pia yanakusudia kuhakikisha shughuli za
zimamoto na uokoaji nchini zinafanyika kwa ufanisi ili kuendelea kuwavutia
wawekezaji kwa kuwahakikishia usalama wa maisha na mali zao; na

Tano: Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.5 wa Mwaka 2021.

  1. Mheshimiwa Spika, nirejee tena kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa
    michango yao mizuri iliyotolewa wakati wa kujadili Miswada hiyo muhimu ambayo itasaidia
    kuondoa mapungufu yaliyobainika sambamba na kuboresha baadhi ya masharti katika
    utekelezaji wa sheria hizo. Serikali itafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa kwa lengo la
    kuhakikisha utekelezaji wa sheria hizo unawanufaisha Watanzania.
  2. Mheshimiwa Spika, niwapongeze na kuwashukuru Waheshimiwa Mawaziri na
    Naibu Mawaziri kwa kazi nzuri ya kuwasilisha Miswada iliyojadiliwa katika mkutano huu
    pamoja na kutoa ufafanuzi mbalimbali wakati wa kujibu hoja za Waheshimiwa Wabunge.
    Aidha, nimpongeze Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wataalamu wake kwa kazi
    nzuri ya kuandaa miswada iliyowasilishwa katika mkutano huu.
  3. MAENEO YA MSISITIZO KISEKTA
  1. Mheshimiwa Spika, jukumu langu la msingi lililonisimamisha mbele ya Bunge lako
    tukufu ni kutoa maelezo mafupi hususan kuhusu shughuli za mkutano huu wa nne wa
    Bunge kabla ya kuahirishwa. Hata hivyo, kabla ya kuhitimisha mkutano huu naomba niweke
    msisitizo wa baadhi ya masuala kwa viongozi, watendaji na wananchi kwa ujumla katika
    kutekeleza majukumu yao ya kuwaletea maendeleo.
  2. Mheshimiwa Spika, baadhi ya maeneo ambayo nitayatolea msisitizo ni suala la
    tozo na uendelezaji wa miundombinu ya afya ya msingi, maandalizi ya uandikishaji wa
    wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2022, matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani,
    ujenzi wa Mji wa Serikali, tahadhari dhidi ya UVIKO-19 na michezo.
    UENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA AFYA YA MSINGI
  3. Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Sera ya Afya ya Mwaka 2007 yenye lengo
    la kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa vituo vya afya na zahanati. Azma ya Serikali ni
    kuona kila kata inapata kituo cha afya na kila kijiji kinakuwa na zahanati ili kusogeza
    huduma hizo karibu na wananchi na kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu. Hadi sasa,
    tarafa 363 zilizopo Tanzania Bara zina vituo vya afya vyenye uwezo wa kutoa huduma za
    upasuaji za dharura, huduma za mionzi na maabara za kisasa.
  4. Mheshimiwa Spika, ili kuzifikia tarafa nyingi zaidi, Serikali imeamua, kwanza
    kuzitambua kata za kimkakati na tarafa zote ambazo hazina vituo vya afya. Pili, kutumia
    fedha zitokanazo na tozo za miamala ya simu kujenga vituo vya afya vya kimkakati
    ambavyo vitakuwa na uwezo wa kutoa huduma za upasuaji za dharura, huduma za mionzi
    na maabara za kisasa katika kata za kimkakati na makao makuu ya tarafa hizo.
  5. Mheshimiwa Spika, hadi sasa Serikali imepeleka shilingi bilioni 37.5 zilizotokana
    na makusanyo ya tozo ya miamala ya simu kwenye Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa vituo
    vya afya kwenye tarafa 150 kati ya tarafa 207. Kila kituo cha afya kimepelekewa shilingi
    milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo. Natoa maelekezo kwa watendaji wote wa
    Serikali za Mitaa kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuakisi
    thamani ya fedha kwenye utekelezaji wa miradi hiyo.
    MAANDALIZI YA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA,
    JANUARI 2022
  6. Mheshimiwa Spika, sote tunafahamu kwamba jana tarehe 9 Septemba, 2021
    vijana wetu wa darasa la saba walimaliza mtihani wa Taifa wa Elimu ya Msingi ulioanza
    tarehe 8 Septemba, 2021. Hivyo basi, nitumie fursa hii kuwapongeza na kuwaombea
    Mwenyezi Mungu awajalie wote wafaulu vizuri na kujiunga na kidato cha kwanza, vyuo vya
    ufundi na kujiendeleza na taaluma nyinginezo.
  7. Mheshimiwa Spika, tangu kuanza kwa utekelezaji wa Sera ya Elimumsingi bila
    Ada kumekuwa na mwitikio mzuri wa mahudhurio ya wanafunzi na hivyo kuongeza idadi ya
    wahitimu katika mitihani ya kujipima na kumaliza elimu ya msingi. Ongezeko hilo la idadi ya
    wahitimu, lilisababisha changamoto ya kutokuwepo kwa miundombinu ya elimu ya kutosha
    hususan madarasa ya kuweza kupokea wahitimu wa darasa la saba waliofaulu kujiunga na
    kidato cha kwanza.

4

  1. Mheshimiwa Spika, kufuatia hali hiyo, Serikali ilitoa maelekezo kwa watendaji wa
    Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatumia takwimu zilizopo kupanga maoteo na kutenga
    fedha katika mipango na bajeti ya kila mwaka ili miundombinu ya elimu, samani na shule
    hitajika viwepo kwa wakati.
  2. Mheshimiwa Spika, maelekezo hayo, yalilenga kuiwezesha Serikali kutambua
    mahitaji ya miundombinu ya elimu yatakayokidhi idadi hiyo ya wanafunzi na hivyo
    kuhakikisha miundombinu hiyo inaandaliwa mapema. Katika mwaka 2021, makadirio
    yanaonesha kuwa wanafunzi 934,706 sawa na asilimia 83.68 ya wanafunzi 1,115,041
    waliohitimu mtihani wa darasa la saba wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza ifikapo
    Januari, 2022.
  3. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika
    shule za sekondari, Serikali imetumia shilingi bilioni 33.73 kwa ajili ya kujenga maboma
    2,699 kati ya maboma 4,539 ya vyumba vya madarasa kwenye maeneo mbalimbali nchini.
    Fedha hizo zinatokana na tozo ya miamala ya simu.
  4. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba tayari
    Serikali imepeleka shilingi bilioni saba kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 560 ikiwa ni
    awamu ya kwanza. Aidha, maboma 1,840 yatakayogharimu shilingi bilioni 23
    yatakamilishwa kupitia ruzuku ya Serikali Kuu.
  5. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kurejea maelekezo niliyoyatoa wakati
    nikifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwamba
    wahakikishe miundombinu hiyo inakamilika kwa wakati. Lengo la Serikali ni kuona vijana
    wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wanapokelewa na kuanza masomo
    yao kwa wakati.
    BEI ELEKEZI YA MAFUTA
  6. Mheshimiwa Spika, tarehe 31 Agosti, 2021 Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati nchini
    (EWURA) ilitangaza bei mpya elekezi kwa bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba ambapo
    ilionesha kupanda kwa bei za bidhaa hizo. Kufuatia taarifa hiyo, na malalamiko ya wananchi
    juu ya kupanda kwa bei za bidhaa hizo, tarehe 1 Septemba 2021, Serikali ilisitisha bei mpya
    zilizotangazwa na EWURA ili kufanya mapitio ya kina ya kupanda huko kwa bei.
  7. Mheshimiwa Spika, tulichukua hatua hizo kutokana na ukweli kwamba kupanda
    kwa bei ya mafuta huwaumiza wananchi hususan wale wa hali ya chini. Kwa kulitambua
    hilo, tarehe 2 Septemba, 2021, niliunda timu maalumu ya uchunguzi.
  8. Mheshimiwa Spika, pamoja na mambo mengine timu hiyo inafuatilia kupanda kwa
    bei za bidhaa za mafuta mara kwa mara hususani petroli, dizeli, mafuta ya taa na ndege na
    kisha kuishauri Serikali hatua stahiki za kuchukuliwa. Aidha, nimeielekeza timu hiyo
    ijiridhishe kuhusu utitiri wa tozo kwenye bidhaa za mafuta na kuja na mapendekezo ya
    namna nzuri ya kushughulikia suala hilo.
  9. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kuwa timu hiyo tayari
    imeanza kutekeleza majukumu yake tangu tarehe 2 Septemba, 2021. Hali kadhalika,
    itakapokamilisha taarifa yake Serikali itatoa mwelekeo wa yale yatakayopendekezwa.

MFUMO WA STAKABADHI ZA MAZAO GHALANI NA USHIRIKA

  1. Mheshimiwa Spika, miongoni mwa maeneo ambayo Serikali inayapa msukumo wa
    kutosha ni masoko na mifumo ya mauzo ya mazao ya wakulima. Serikali inachukua hatua
    hizi ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata tija na kunufaika na mazao yao. Katika
    kutimiza azma hiyo, Serikali imeondoa mifumo isiyo rasmi ya ununuzi wa mazao ambayo
    imekuwa ikiwakandamiza wakulima na kuwanufaisha baadhi ya wanunuzi wasiokuwa
    waaminifu. Mathalan, tuliondoa mifumo kama vile kangomba, butula, chomachoma,
    kula maua, njemke na mingineyo ambayo ilikuwa ikimpunja na kumnyonya mkulima.
  2. Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hiyo, Serikali imekuwa ikisimamia kikamilifu
    mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani ambao umeonesha mafanikio makubwa katika
    uuzaji wa mazao yakiwemo korosho, ufuta, dengu, choroko na kakao. Kwa lugha nyingine,
    ufanisi wa mfumo huo, umekuwa kichocheo katika kupunguza umaskini na kuongeza
    uchumi wa nchi na wakulima kwa ujumla.
  3. Mheshimiwa Spika, taarifa zinaonesha kuwa kuuza mazao kupitia mfumo wa
    stakabadhi ghalani na ushirika kunatoa nguvu ya pamoja kwa wakulima katika upatikanaji
    wa masoko sambamba na kuimarisha bei ya mazao husika. Minada iliyofanyika imesaidia
    kuongezeka kwa bei ya mazao yaliyotumia mfumo wa stakabadhi ghalani ikiwemo
    korosho, ufuta, dengu, choroko na kakao.
  4. Mheshimiwa Spika, mwaka 2020 bei ya choroko iliongezeka kutoka shilingi 600
    kwa kiwango cha chini hadi 800 kiwango cha juu kwa kilo na kufikia shilingi 900 hadi
    1,300 kwa kilo katika vituo vya Magu, Uzogele, Igunga na Manyoni. Kadhalika, hivi
    karibuni tumeona bei ya kakao ikiongezeka maradufu kutoka shilingi 2,500 hadi 5,000
    kwa kilo baada ya kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani.
  5. Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo, natoa maelekezo kwa Wizara ya Kilimo
    kushirikiana kwa karibu na vyama vya ushirika na vyama vya msingi katika kuhakikisha
    wanawawezesha wakulima kupata elimu na manufaa ya kutumia mfumo wa stakabadhi
    ghalani bila usumbufu ili uwapatie tija.
  6. Mheshimiwa Spika, ni kweli mfumo wa stakabadhi ghalani unahitaji miundombinu
    ya maghala. Hata hivyo, changamoto hizo zinaendelea kufanyiwa kazi ili mazao mengi zaidi
    yaingizwe kwenye mfumo huo mwaka hata mwaka na kuleta tija zaidi kwa wakulima.
  7. Mheshimiwa Spika, rai yangu kwa wakulima na wanunuzi wa mazao ni kwamba,
    mfumo wa stakabadhi ghalani ndiyo pekee uliothibitika na kuonesha matokeo makubwa
    yenye manufaa. Hivyo basi, tuendelee kuuimarisha katika mazao yote ya biashara nchini ili
    kuleta mafanikio kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
    UNUNUZI WA NAFAKA NCHINI
  8. Mheshimiwa Spika, Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhamasisha
    uzalishaji wa mazao ya chakula hususan nafaka pamoja na mazao ya biashara. Ongezeko
    hili la uzalishaji linakwenda sambamba na jitihada za Serikali za kuimarisha masoko ya
    ndani ya mazao pamoja na kutafuta masoko ya nje.
  9. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuboresha mifumo ya masoko, Serikali
    inahamasisha ujenzi wa viwanda vya uchakataji wa mazao yanayozalishwa hapa nchini ili
    kuimarisha bei ya mazao hayo na hivyo kumpatia tija mkulima.

  1. Mheshimiwa Spika, baada ya kuanza kwa msimu wa ununuzi wa mahindi hususan
    katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, tulipokea malalamiko ya wananchi kuhusu umbali wa
    vituo vya kununulia mahindi na bei kutoridhisha. Kama mnavyofahamu, kwa kiasi kikubwa
    ununuzi wa mahindi nchini hufanywa na wafanyabiashara binafsi. Hata hivyo, ili kuimarisha
    bei ya mahindi, Serikali hutoa fedha kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na
    Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB).
  2. Mheshimiwa Spika, jana tarehe 9 Septemba 2021, Bunge lako tukufu lilipokea
    hoja binafsi kutoka kwa Mheshimiwa Justin Nyamoga, Mbunge wa Kilolo na kuungwa
    mkono na Waheshimiwa Wabunge. Hoja hiyo, ililenga kuishauri Serikali kuingilia kati soko la
    mahindi ili kunusuru wakulima wa zao hilo.
  3. Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa shilingi bilioni 15 kwa ajili kuwezesha Wakala
    wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua mahindi maeneo mbalimbali nchini. Pia,
    Serikali ilitoa kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko shilingi bilioni 10 kuongeza
    mtaji wa ununuzi wa mazao.
  4. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa kiasi hicho cha fedha ni kidogo
    ukilinganisha na uzalishaji wa mahindi uliopo. Hivyo, Serikali imesikia kilio cha wakulima
    kupitia Waheshimiwa Wabunge na kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wakulima
    wa mahindi wanapata soko la mahindi waliyozalisha.
  5. Mheshimiwa Spika, tayari Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
    Muungano wa Tanzania, ametoa shilingi bilioni 50 na ununuzi utaanza Jumatatu, tarehe
    13 Septemba, 2021. Hivyo, Wizara iendelee kutafuta masoko ya mahindi kwa
    kukamilisha mikataba mipya ya ununuzi wa mahindi na nchi za Sudan ya Kusini, DRC na
    Zimbabwe.
  6. Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeruhusu wafanyabiashara kutafuta masoko ya
    nje ya nchi ambapo vibali vya usafirishaji hutolewa kupitia Ofisi za Wakuu wa Wilaya. Aidha,
    uuzaji wa chakula utafanywa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na
    hifadhi ya kutosha ya chakula. Niendelee kusisitiza Wizara kushirikiana na Sekta Binafsi
    katika kuongeza thamani ya mazao yetu ikiwemo mazao ya nafaka badala ya kuyauza nje
    yakiwa hayajaongezwa thamani.
  7. Mheshimiwa Spika, naiagiza Wizara ya Kilimo kuisimamia kwa karibu NFRA na CPB
    ili zinunue mahindi ya wakulima pekee, tena watoke ndani ya nchi. Aidha, ongezeni vituo
    vya kununulia mahindi hadi wilayani na kwenye miji midogo.
  8. Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, Serikali inafuatilia mwenendo wa
    upatikanaji wa mbolea ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana kwa wingi na bei nafuu.
    Lengo la Serikali ni kuwezesha wakulima kumudu gharama za mbolea.
    UJENZI WA MJI WA SERIKALI
  9. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa Mji wa Serikali, mradi ambao
    unatekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Itakumbukwa kuwa katika awamu ya kwanza, Wizara
    23 zilijenga ofisi zake na kuhamishia watumishi wapatao 18,300 jijini Dodoma. Aidha,
    ujenzi wa majengo ya kudumu ya wizara 23 na taasisi zake utaanza tarehe 30 Septemba,
  10. Ujenzi huo, utahusisha ipasavyo kampuni za ujenzi za umma na binafsi.

  1. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa
    Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia shilingi
    bilioni 300 zitumike katika awamu ya pili ya ujenzi huo. Kadhalika, shilingi bilioni 300
    nyingine zitatolewa kadri ujenzi unavyoendelea. Hivi sasa, ujenzi wa miundombinu wezeshi
    ikiwemo barabara, majisafi na majitaka, umeme, gesi, mifumo ya TEHAMA, huduma za
    zimamoto na upandaji miti unaendelea vizuri na kasi kubwa.
    TAHADHARI DHIDI YA UVIKO-19
  2. Mheshimiwa Spika, Tanzania na dunia kwa ujumla bado imeendelea kupambana
    na ugonjwa wa virusi vya korona maarufu kama UVIKO-19. Janga limesababisha baadhi ya
    ndugu zetu kupoteza maisha na wengine kuendelea kuugua. Hivyo basi, hatuna budi
    kuendelea kuchukua tahadhari kwa kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19.
  3. Mheshimiwa Spika, ninawasihi Waheshimiwa Wabunge wenzangu na wananchi
    wote, tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na pale mtu anapoona dalili
    ambazo hazielewi, awahi kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu ili
    afanyiwe uchunguzi na kupatiwa matibabu.
  4. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine ya kukabiliana na UVIKO-19, tarehe 28
    Julai, 2021 Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
    alizindua rasmi kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Hivi sasa, chanjo hiyo inapatikana
    maeneo yote nchini katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya afya wilayani na
    mikoani.
  5. Mheshimiwa Spika, niwatoe hofu Waheshimiwa Wabunge wenzangu na wananchi
    wote kuwa chanjo hii ni salama na haina madhara yoyote. Chanjo hiyo ambayo
    imethibitishwa na watalaamu na maabara zetu, ni hiyari lakini ni muhimu. Hivyo, niwaombe
    twendeni tukachanje ili kukabiliana na janga hili.
    MATUMIZI YA MITANDAO
  6. Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kumejitokea tabia ya baadhi ya watu kutumia
    vibaya haki ya uhuru wa mawazo na mifumo mbalimbali ya mawasiliano. Matumizi mabaya
    ya mitandao yamesababisha kusambazwa kwa taarifa za upotoshaji, kashfa, kutisha, na
    wakati mwingine kudhalilisha watu, kikundi au viongozi.
  7. Mheshimiwa Spika, katika kulinda na kutunza usalama, amani, maadili, umoja na
    mshikamano wa nchi ninawaagiza Mawaziri wa Mambo ya Ndani na mwenzake wa Habari
    na Teknolojia ya Mawasiliano watumie sheria, kanuni na taratibu zilizopo kuhakikisha
    vitendo na mienendo hiyo inadhibitiwa nchini.
    MICHEZO
  8. Mheshimiwa Spika, nyote mtakubaliana nami kwamba kumekuwepo na mwamko
    mkubwa wa masuala ya sanaa, burudani na michezo nchini. Hivi sasa, michezo imekuwa
    chanzo kikubwa cha biashara, utalii, kuimarisha afya na ajira kwa vijana wetu. Kwa
    kuzingatia hilo, Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi za kukuza michezo nchini.
    Hatua hizo zinahusisha kuundwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo na kurejesha
    mashindano ya UMITASHUMTA, UMISSETA na SHIMIWI.

  1. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu
    Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia kuanzishwa kwa Mfuko
    wa Maendeleo ya Michezo nchini na kukubali kudhamini mashindano ya wanawake ya
    CECAFA ili kutoa motisha kwa wanawake kushiriki zaidi katika michezo. Mashindano hayo,
    yatajulikana kama Samia Cup sambamba na Kagame Cup kwa upande wa wanaume.
  2. Mheshimiwa Spika, Mfuko huo, utasaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya
    kuziandaa vyema timu zetu za Taifa za michezo mbalimbali na kuziwezesha kushiriki kwa
    tija katika mashindano na michezo ya kimataifa. Pia, utatumika kuimarisha miundombinu ya
    michezo na upatikanaji wa vifaa vya michezo, kuendeleza na kuwezesha shule na vituo vya
    umahiri wa michezo, kuendesha programu za mafunzo ili kupata wataalaamu wa kutosha,
    kuwezesha programu za michezo kwa jamii na mashindano ya kitaifa na kimataifa.
  3. Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kueleza, michezo ni biashara na imekuwa
    chanzo muhimu cha ajira hususan kwa vijana. Aidha, ibara ya 243 ya Ilani ya Uchaguzi ya
    Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 inaielekeza Serikali kuanzisha mfumo thabiti wa
    michezo ya kulipwa ili kulinda na kuendeleza vipaji vilivyopo kwa manufaa ya Taifa letu na
    vijana kujipatia ajira kwa kutumia vipaji vyao. Tayari, Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa
    (BMT) imefanyiwa mabadiliko na kuruhusu michezo ya kulipwa na baadhi ya timu zetu
    zimeshaingia kwenye mfumo huo.
  4. Mheshimiwa Spika, kutokana na utekelezaji wa sheria hiyo, hivi karibuni,
    tumeshuhudia watalaamu wa michezo na wachezaji kutoka katika mataifa makubwa
    yaliyoendelea kimichezo wakija nchini kutafuta ajira kupitia michezo. Vilevile, tumeshuhudia
    uwekezaji mkubwa kwenye vilabu vyetu vikubwa nchini hususan Azam, Simba na Yanga na
    kuvifanya viendeshwe kibiashara.
  5. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kwanza kuupongeza uongozi wa Shirikisho la
    Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Wallace Karia kwa usimamizi mzuri wa soka nchini. Pili,
    nawapongeza sana wawekezaji na watendaji wa vilabu vya Azam, Simba na Yanga kwa
    uwekezaji mkubwa na usimamizi mzuri wa vilabu hivyo kwenye soka letu ambao umeanza
    kuzaa matunda.
  6. Mheshimiwa Spika, ninataka niwahakikishie wadau na wapenzi wa michezo kuwa
    Serikali itaendelea kuimarisha na kuvutia uwekezaji mkubwa katika tasnia ya michezo.
    Lengo ni kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu kimichezo ili waweze kushindana
    katika masoko ya michezo ya ndani na nje ya nchi, na hivyo kuimarisha ajira, mapato
    yatokanayo na shughuli za michezo pamoja na mchango wa sekta ya michezo katika pato la
    Taifa.
  7. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuipongeza timu yetu ya Taifa ya Mpira wa
    Miguu (Taifa Stars) kufuatia ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Madagascar na
    hivyo kuongoza KUNDI J katika hatua ya pili ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwakani
    nchini Qatar. Vilevile, tunaitakia kila la heri timu yetu ya wanawake ya kriketi inayoshiriki
    mashindano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia la mchezo huo nchini Botswana na timu
    yetu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) itakayoshiriki mashindano ya COSAFA nchini
    Afrika Kusini kuanzia tarehe 28 Septemba, 2021 pamoja na kuitakia mafanikio timu yetu ya
    mchezo wa wavu inayoendelea kushiriki mashindano ya Afrika ya mchezo huo nchini
    Rwanda. Ninavitakia kila la heri pia vilabu vyetu vya Azam, Biashara United, Simba na

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia kukipongeza kituo cha matangazo cha
Azam (Azam Media) hususan upande wa matangazo ya runinga kwa kuuibua na
kuutangaza vyema mchezo wa masumbwi nchini. Juhudi hizo za Azam Media
wakishirikiana na wadau wengine zimewezesha wanamasumbwi wetu kutumia vizuri fursa
hiyo kukuza vipaji vyao.

Mheshimiwa Spika, niwapongeze mabondia wetu Twaha Kiduku kwa kumtwanga
Dulla Mbabe katika pambano lililovuta hisia za Watanzania wengi. Vilevile, nimpongeze
bondia Hassan Mwakinyo kwa kumdunda mpinzani wake Mnamibia Julius Indongo kwa TKO
na kutetea mkanda wake wa Chama cha Ngumi Afrika (ABU). Wanamasumbwi wetu
wameendelea kuifanya Tanzania itambulike zaidi ulimwenguni. Sasa tunasubiri pambano la
watani Mwakinyo dhidi ya Kiduku.
HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, nihitimishe hotuba yangu kwa kumshukuru Katibu wa Bunge
na watendaji wa ofisi ya Bunge kwa kazi kubwa ya kuratibu vikao vya mkutano huu. Aidha,
niwashukuru watendaji wa Serikali kwa kufanikisha shughuli zilizopangwa na Bunge lako
tukufu kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, kipekee, niwashukuru wanahabari kwa kufikisha habari
kuhusu mkutano huu kwa wananchi. Nivishukuru pia vyombo vya ulinzi na usalama kwa
huduma wanazozitoa kwa washiriki wa Bunge hili bila kuwasahau madereva
waliotuhudumia wakati wote tukiwa hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, natambua kuwa baada ya mkutano huu Waheshimiwa
Wabunge wenzangu watakuwa wakirejea majimboni kwao kuendelea na shughuli za
kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kuwaeleza mambo yaliyojiri hapa Bungeni. Kwa
hiyo, niwatakie safari njema na niwaombe kuwa mkawaeleze wananchi pia kuhusu
matarajio yetu kwao na kuwasihi waendelee kutuunga mkono kusukuma mbele gurudumu
la maendeleo.

Mheshimiwa Spika, tarehe 19 Oktoba 2021, ikitegemewa na mwandamo wa
mwezi, ndugu zetu Waislamu wataadhimisha Mazazi ya Mtume Muhammad Swalla Allahu
Alayh Wasallam. Hivyo, nitumie nafasi hii kuwatakia kila la heri katika maandalizi na
hatimaye maadhimisho ya shughuli hiyo ya maulid ya kuadhimisha Mazazi ya Mtume
Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasa, naomba kutoa hoja kwamba
Bunge lako tukufu liahirishwe hadi tarehe 2 Novemba, 2021 siku ya Jumanne, saa tatu
kamili asubuhi litakapokutana tena katika ukumbi huu jijini Dodoma.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Yanga katika uwakilishi wao kwenye michuano ya Shirikisho na Ligi ya Mabingwa ya Chama
cha Soka barani Afrika (CAF).

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »