TFF NA WIZARA YA MAJI KUKUZA MICHEZO NCHINI

TFF NA WIZARA YA MAJI KUKUZA MICHEZO NCHINI

NA MWANDISHI-MOROGORO. SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini(TFF) kwa kushirikiana na Wizara za Maji wameanzisha mashindano ya mpira wa miguu yanayozihushisha Mamlaka za Maji nchini (Maji Cup) ili kuhakikisha mamlaka hizo zinakuwa na timu zao. Hayo yalisemwa na Meneja wa soka la vijana wa TFF Boniface Pawasa mkoani hapa ambapo alizipongeza mamlaka hizo za maji


NA MWANDISHI-MOROGORO.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini(TFF) kwa kushirikiana na Wizara za Maji wameanzisha mashindano ya mpira wa miguu yanayozihushisha Mamlaka za Maji nchini (Maji Cup) ili kuhakikisha mamlaka hizo zinakuwa na timu zao.

Hayo yalisemwa na Meneja wa soka la vijana wa TFF Boniface Pawasa mkoani hapa ambapo alizipongeza mamlaka hizo za maji za mkoa ya Morogoro,    Dodoma na Singida kwa kuanzisha mashindano hayo ili kukuza soka nchini.

“Nimefurahishwa na kitendo hiki cha mamlaka za maji mikoa ya Morogoro,Dodoma na Singida kuandaa mashindano ya Maji Cup kwa lengo la kupata timu zitakazoshiriki ligi mbambali hapa nchini”alisema Pawasa.

Pawasa alisema kitendo hicho kitasaidia sana kukuza soka la Tananzia lakini poa kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya soka ambapo alieleza kuwa TFF itakuwa mstari wa mbele katika kutoka ushirikiano ili kuhakikisha azma hiyo inafanikiwa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya maji nchini (ATAWAS) Costantino Chiwaligo alisema lengo ni kuwa na timu za mpira wa miguu na mpira wa pete ambazo zitashiriki ligi kuu ili kuongeza ajira kupitia taasisi za serikali.

“Mshindano haya ni ya muhimu kwetu,tumedhamilia kuwa na timu ya mpira wa miguu pamoja na wa pete ambazo zitashiriki ligi kuu Tanzania Bara ili kuongeza ajira ya michezo hiyo hapa nchini kupitia Mamlaka za Maji”alisema Chiwaligo.

Katika mashindano hayo ambayo pia yaliendana na kampeni ya kutokomeza upotevu wa maji,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingia Morogoro(MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba alitumia wasaa huo kukemea  vitendo vya rushwa mahala pa kazi.

Mhandishi Katakweba alikemea vitendo vya rushwa kwa watumishi wote wa mamlaka hizo ikiwa ni pamoja na kuepuka tabia ya kuwabandikia bili wateja wa maji siyostahili pia aliwataka kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mwili yao.

Kwa upande wake Kocha timu ya DUWASA Khalifa Ibrahimu mbali na kuwapengeza MORUWASA kwa mchezo mzuri pia alisema mashindano hayo yatasaidia kuwaunganisha watumishi wa mamkala kwani wa ni baba mmoja.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »