MAMLAKA ZA MAJI KUKABILIANA NA UPOTEVU WA MAJI

MAMLAKA ZA MAJI KUKABILIANA NA UPOTEVU WA MAJI

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO. MAMLAKA za Maji mikoa ya Morogoro,Dodoma na Singida imeanzisha kampeni ya kutokomeza upotevu wa maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu bila kuwa na changamoto yoyote na kwa bei nafuu. Hayo yalisema na Mkurugenzi wa Maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba


NA MWANDISHI WETU, MOROGORO.

MAMLAKA za Maji mikoa ya Morogoro,Dodoma na Singida imeanzisha kampeni ya kutokomeza upotevu wa maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu bila kuwa na changamoto yoyote na kwa bei nafuu.

Hayo yalisema na Mkurugenzi wa Maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba ambapo alisema kuwa kitendo cha kupambana na upotevu wa maji ni hazina kwa taifa.

“Kumekuwa na changamoto ya upotevu wa maji unaofanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo wizi wa maji ikiwa ni pamoja na mvujo na kusababisha mamlaka za maji kupata hasara hivyo tumeamua kukabiliana sana na tatizo hili ”alisema Katakweba.

Katakweba alisema kitendo cha mvujo wa maji husababisha baadhi ya watu kutopata huduma ya maji ya uhakika lakini pia yanapokuwa yakipatikana huwa na gharama kubwa kitendo ambacho kimekuwa kikisababisa kero kwa wananchi.

Alisema kuwa serikali kupitika Wizara ya Maji imeziagiza mamlaka ya maji kuhakikisha changamoto zote za maji zinatatuliwa ili wananchi waondokane na kero ya hiyo hali itakayosaidia sana kuwatua wanawake ndoo za maji kichwani.

Aidha Mhandisi Katakweba aliwataka wananchi wote kuwa walinzi dhidi ya wanaohujumu miundombinu ya maji kwa kutoa taarifa kwa mamlaka za maji ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa kwa wote wakaobainika kuhusika na hilo.

Katakweba aliwataka watumishi wa mamlaka za maji katika mikoa hiyo kuwa wazalendo kwa taifa lao na kuepuka kuwapandikia wateja bili za maji,kuepuka rushwa ikiwa ni pamoja kuwa na tahadhari kubwa dhidi ya magonjwa yote hatari.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano ya Umma Mamlaka ya Maji mkoa wa Sindiga James Malima alisema utopevu wa maji ni adui mkubwa kwa mamlaka hizo za maji hivyo wameamua kukabiliana na tatizo hilo nchini.

Malima aliwataka wasoma mita wote mikoa ya Morogoro,Dodoma na Sindiga ikiwa ni pamoja na mikoa yote nchini kuacha tabia ya kuwabandikia bili wateja kwani kitendo hicho hakileti picha nzuri kwa mamlaka hivyo wawe waadilifu.

Alex Mpagana ni Meneja Biashara wa Mamlaka ya Maji mkoa wa Dodoma(DUWASA) aliishukuru ushirikiano wa Wizara ya Maji ambapo alisema kampeni hiyo itasaidia sana kupunguza changamoto ya upotevu wa maji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »