AJALI YA MASHUA MAFIA, MMOJA ANUSURIKA KATI YA ABIRIA SITA WALIOKUWEMO.

AJALI YA MASHUA MAFIA, MMOJA ANUSURIKA KATI YA ABIRIA SITA WALIOKUWEMO.

Mashua ijulikanayo kama ‘MV Adui Jamaa (Mbagara)’ imepata ajali na kuzama katika eneo la Simani (Songosongo) siku ya Jumatano ya tarehe 08 Septemba, 2021. Mashua hiyo ilikuwa na mzigo wa mwani ikiusafirisha kutoka kisiwa cha Jibondo wilayani Mafia kuelekea Kilwa. Jumla ya watu sita walikuwa katika mashua hiyo ambapo wanne kati yao walikuwa ni wafanyakazi

Mkuu wa wilaya ya Mafia Eng. Martin Ntemo


Mashua ijulikanayo kama ‘MV Adui Jamaa (Mbagara)’ imepata ajali na kuzama katika eneo la Simani (Songosongo) siku ya Jumatano ya tarehe 08 Septemba, 2021.

Mashua hiyo ilikuwa na mzigo wa mwani ikiusafirisha kutoka kisiwa cha Jibondo wilayani Mafia kuelekea Kilwa. Jumla ya watu sita walikuwa katika mashua hiyo ambapo wanne kati yao walikuwa ni wafanyakazi na wawili ni abiria.

Mkuu wa wilaya ya Mafia Eng. Martin Ntemo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo mara baada ya kupokea taarifa hizo za kusikitisha aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kwa kushirikiana na wadau wengine, kwenda katika eneo ilipotokea ajali ili taratibu za uokoaji zichukuliwe mara moja. Abiria mmoja aliyetambulika kwa jina Saidi Twalibu aliokolewa akiwa hai.

Wataalam kutoka Hifadhi ya Bahari Mafia (HIBAMA) waliongoza zoezi la uokoaji. Msako huo ulidumu kwa siku tatu mfululizo hadi maiti tatu zilipopatikana maeneo ya Rufiji na Kilwa.

Miili iliyopatikana imetambuliwa kuwa ni Amri saidi Amri (Ngenje) aliyekuwa nahodha wa chombo kilichopata ajali na Sadiki Abdallah Apondo ambao wote wamepatikana na kuzikwa katika kijiji cha Pombwe wilayani Rufiji. Mwili mwingine ni wa Selemani Faki Hassani (Mnyaku) ambaye amezikwa katika kijiji cha Somanga wilayani Kilwa.

Jitihada zinaendelea za kuwatafuta wahanga wengine wawili ambao ni Hamza Shahame na Ahmadi Mwinyimanga, hatma yao bado haijajulikana.

Mkuu wa Wilaya ameelezea kusikitishwa kwake kwa kutokea ajali hiyo na anaungana na ndugu na jamaa wote waliopoteza wapendwa wao. Amewasihi wamiliki na maendesha vyombo vya usafiri majini kuhakikisha wanazingatia masuala ya usalama hasa kwa kutozidisha uzito, kukagua mara kwa mara ubora wa vyombo vyao na kufuata miongozi mbali mbali inayotolewa na wataalam ikiwa nipamoja na hali ya hewa.

Na Scolastica Msewa

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »