Mhe. Hemed amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kuwachukulia hatua watendaji wa CCM wasio waaminifu .

Mhe. Hemed amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kuwachukulia hatua watendaji wa CCM wasio waaminifu .

Mlezi wa Mkoa wa Tanga ambae pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi Pamoja na wanachama wa wilaya ya Handeni katika Ukumbi wa Mikutano wa Makuti uliopo Handeni Mjini. Katika kulitekeleza hilo Mhe. Makamu wa Pili wa Rais alimtaka Mkuu wa Mkoa

MKOA WA KUSINI PEMBA

Mlezi wa Mkoa wa Tanga ambae pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi Pamoja na wanachama wa wilaya ya Handeni katika Ukumbi wa Mikutano wa Makuti uliopo Handeni Mjini.

Katika kulitekeleza hilo Mhe. Makamu wa Pili wa Rais alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kuwachukulia hatua watendaji wake wasiokuwa waaminifu kwa lengo la kuhakikisha ilani CCM inatekelezwa Vyema.

Akizungumza katika kikao hicho cha ndani Mhe. Hemed aliwakumbusha viongozi hao kuachana na tabia ya makundi kupitia uchaguzi uliomalizika mwaka 2020 ili kuwapa fursa viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kuwatumikia wanachi katika maeneo yao.

Mapema asbuhi mjumbe huyo wa kamati kuu alitembelea shina nambari tano kata ya kivesa wilaya ya Handeni na kusalimiana na Wanachama.

Akiwa katika eneo hilo viongozi mbali mbali akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Handeni walimuleza mlezi huyo juu ya Faraja yao kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania  kuwa.

Wakati wa Mchana Makamu wa Pili wa Rais alishiriki katika ujenzi wa kituo cha Afya Sendeni ambapo kituo hicho kitakapokamilika kinatarajiwa kuwahudumia wananchi takribani Laki Tatu wa wilaya ya handeni.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo mganga mkuu wa Afya Wilaya KANASIA MICHEL SHOO  alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kwamba

Wakati wa Jioni Mhe. Hemed alikfika katika wilaya ya Korogwe katika eneo la skuli ya Sekondari ya  JOEL BENDERA na kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa maabara Pamoja na ufungua vyumba viwili vya madarasa ya kusomea wanafunzi.

Akikagua mradi huo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu aliwaagiza wasimamizi wa ujenzi huo kufanya baadhi ya marekebisho kwa madawati ili kutoa huduma nzuri kwa wananfunzi wa Skuli hiyo.

Ziara hiyo ya Mlezi wa Mkoa wa Tanga inatarajiwa kuendelea kesho katika wilaya ya Korogwe na Wilaya ya Muheza ambapo Mhe. Hemed atetembelea miradi mbali mbali ikiwemo miradi ya miundombinu ya Barabara.

……………………………..

Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

24/09/2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »