BIHIMBA ATUA MSONGOLA ORPHANAGE, ATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA

BIHIMBA ATUA MSONGOLA ORPHANAGE, ATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA

 Na Mwandishi Wetu. Mwanaharakati Huru nchini Tanzania Bwana Bihimba Nassoro Mpaya Jana alitembelea kituo cha Watoto Yatima cha MSONGOLA ORPHANAGE TRUST FUND kilichopo Ilala Jijini Dar Es Salaam na kutoa Misaada mbalimbali kwa Watoto Yatima wanaolelewa katika kituo hicho. Akizungumza wakati wa kutoa Misaada hiyo Bwana Bihimba amewasihi  watoto hao kwamba  wasivunjike mioyo  kwa kuishi yatima

 Na Mwandishi Wetu.

Mwanaharakati Huru nchini Tanzania Bwana Bihimba Nassoro Mpaya Jana alitembelea kituo cha Watoto Yatima cha MSONGOLA ORPHANAGE TRUST FUND kilichopo Ilala Jijini Dar Es Salaam na kutoa Misaada mbalimbali kwa Watoto Yatima wanaolelewa katika kituo hicho.

Akizungumza wakati wa kutoa Misaada hiyo Bwana Bihimba amewasihi  watoto hao kwamba  wasivunjike mioyo  kwa kuishi yatima na badala yake wasome kwa bidii , maana hata yeye mwenyewe (Bwana Bihimba ) ni moja kati yao maana alipoteza wazazi wake akiwa na umri mdogo sana (Darasa la Tatu)

“Ahsante Sana Mungu kwa siku ya Leo kunipatia Afya na Uzima,  nimeweza kufika katika Kituo Cha Kulelea Watoto yatima, kilichopo kata ya Msongola chenye Watoto 48 kwa sasa, Leo nimeweza Tena kukabidhi, Vyakula mbalimbali na Vifaa vya Shule vya Watoto ambavyo ni Mchele kilo50, Unga kilo25,  sukari kilo10,  Nyama kilo5,  Maharage kilo10,  Daftari50,  kalamu50, na  Mikate ,nilicho waambia wasifunjike Moyo kwa kuishi yatima,Muda wa Mungu ndio muda sahihi” Alisema Bwana Bihimba.

Mwanaharakati Bihimba Mpaya (kulia), katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Msongola Orphanece Trust Fund.

 Bihimba Mpaya  aliongezea  kuwa watoto yatima wanaolelewa katika vituo vya Kulelea watoto  hao wanahitaji faraja  ili wajione hawajatenga na jamii na kumalizia kwa kutoa Wito kwa Jamii , Taasisi na watu mmoja mmoja wanaojiweza waweze kuiga alichokifanya 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »