Waumini wa Dini ya Kislamu wametakiwa kujitolea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi na maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa.

Waumini wa Dini ya Kislamu wametakiwa kujitolea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi na maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa.

Waumini wa Dini ya Kislamu wametakiwa kuendelea kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha ujenzi na maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa inayotarajiwa kunza Ijumaa Oktoba 22  wiki hii. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo wakati akikagua na kushiriki katika harakati za ujenzi wa Mskiti wa Ijitimai Kidoti Mkoa

Waumini wa Dini ya Kislamu wametakiwa kuendelea kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha ujenzi na maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa inayotarajiwa kunza Ijumaa Oktoba 22  wiki hii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo wakati akikagua na kushiriki katika harakati za ujenzi wa Mskiti wa Ijitimai Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mhe. Hemed amewakumbusha waumini kuendelea kujitolea katika kukamilisha harakati za ujenzi wa mskiti mkubwa unaojengwa katika eneo la Kidoti ili uweze kutoa tija kwa waislamu Nchini na duniani kwa ujumla.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa mskiti huo pamoja na vituo vya kutolea taaluma kutaisaidia serikali kwa kiasi kikubwa kurekebisha tabia za watu kwa kuachana na vitendo viovu akitolea mfano vitendo vya udhalilishaji na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

“Kuwepo kwa Kituo hichi kusaidia kujenga maadili ya mema ya watu wetu” Alisema Mhe. Hemed

Aidha Makamu wa Pili wa Rais ametumia fursa hiyo kuwapongeza waumini kwa kujitolea kwao katika kufanikisha ujenzi huo wakiwmo akina mama ambapo wamefikia takribani ya asilimia Sabiini (70%) katika maendeleo ya ujenzi huo.

Wakati akiendelea kukagua maendeleo ya ujenzi huo amelezea kuridhishwa kwake ambapo amejitolea kuchangia jumla ya Mifuko Miatu ya saruji ili kumalizia zoezi la utiaji wa floo kwa eneo lililosalia pamoja kuchangia polo hamsini za mchele kwa ajili ya Chakula katika Ijimai inayotarajiwa kuanza Ijumaa ya wiki hii.

Nae, Katibu wa Jumuiya ya Fisabililah Markazi Sheikh Mwalimu Hafidhi Jabu amemueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri ambapo Jumuiua ya Fisabililah Markazi inakusudia kujenga Maktaba kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kuweka vitabu vya dini ya kislamu ili kuwawezesha waumini kupata vitabu vya rejea.

Ijitimai ya Kimataifa ya mwaka huu inatarajiwa inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-Haji Dk. Hussein Ali Mwinyi na kufungwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Samahatu Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ally Mbwana.

………………………….

Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

19/10/2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »