Prof. Shemdoe amewaagiza washiriki wa mechezo ya Wizara na Idara za Serikali kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma .

Prof. Shemdoe amewaagiza washiriki wa mechezo ya Wizara na Idara za Serikali kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma .

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza washiriki wa mechezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI kufuata sheria, taratibu za utumishi wa umma kuzingatia maadili katika kipindi chote cha mashindano ili kupata ushindi uliotukuka. Prof. Shemdoe alitoa agizo hilo Oktoba

May be an image of 2 people, people sitting, people standing and indoor
May be an image of 1 person, sitting and indoor

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza washiriki wa mechezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI kufuata sheria, taratibu za utumishi wa umma kuzingatia maadili katika kipindi chote cha mashindano ili kupata ushindi uliotukuka.

Prof. Shemdoe alitoa agizo hilo Oktoba 18, 2021 Jijini Dodoma na kuwataka timu zote za Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha inacheza kwa kujituma, bidii na nidhamu ili irudi na ushindi wa kishindo katika michezo yote itakayoshiriki.

“Nina imani na sina wasiwasi na mashindano hayo mnayoenda pia tuna uwakilishi mzuri wa timu ya netball na juzi tu wa mekuja na Kombe la Nyerere CUP ambalo tumechukua ushindi wa Kitaifa” alisema Prof. Shemdoe.

Amesema kuwa michezo ya SHIMIWI ni muhimu kwa sababu kwa kuwa inawakutanisha taasisi na Wizara za Serikali zote na inasaidia kuboresha afya na kuongeza hamasa ya utendaji kazi hivyo kuongeza tija na ufanisi wa kazi.

Alisisitiza kwa kuwataka wachezaji hao kuzingatia nidhamu katika michezo na maisha watakayokwenda kuishi kwa kipindi chote watakacho kuwa huko kwenye michezo kwa kujilinda na kujitunza kwani kuna mangonjwa.

Naye Mkurugenzi wa Utawala za Rasilimali watu Victor Kategere amesema jumla ya washiriki 60 wanategemewa kushiriki michezo hiyo ambao watashiriki katika riadha, kuvuta kamba, mpira wa kikapu na Mpira wa Miguu na kusisitiza kuwa washiriki wote wapo vizuri kwa ushiriki.

Kwa upande wake Katibu wa Tamisemi Sports Club Bwana Alex Moris ameahidi kurudina ushindi kwa kuwa timu imejiandaa vizuri na ipo tayari kwa kwenda kushindana na kurudi na ushindi.

Mashindano wa SHIMIWI mwaka huu yanafanyika Mkoani Morogoro na yanatarijiwa kufunguliwa tarehe 20/10/2021 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »