TIGO PESA KIBUBU YAZIDI KUWANUFAISHA WATEJA WA TIGO

TIGO PESA KIBUBU YAZIDI KUWANUFAISHA WATEJA WA TIGO

Na Mwandishi wetu Baadhi ya wateja wa Tigo Wameendelea kuisifia Huduma ya mfumo wa Kidigitali wa Huduma za Kifedha kupitia simu za Mkononi ambao unawawezesha wateja kuweka akiba ya kiwango fulani cha fedha za kielektroniki (e- money) na kujipatia riba kulingana na Kiwango cha fedha kilichohifadhiwa maarufu kama “TIGO PESA KIBUBU”. Wakizungumza kwa Nyakati tofauti

Na Mwandishi wetu

Baadhi ya wateja wa Tigo Wameendelea kuisifia Huduma ya mfumo wa Kidigitali wa Huduma za Kifedha kupitia simu za Mkononi ambao unawawezesha wateja kuweka akiba ya kiwango fulani cha fedha za kielektroniki (e- money) na kujipatia riba kulingana na Kiwango cha fedha kilichohifadhiwa maarufu kama “TIGO PESA KIBUBU”.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti tofauti Bwana Hamis Omary ( Dereva Bodaboda) na Ally Juma Omary ( muuza mitumba) wameelezea ni kwa namna gani huduma hii ya Tigo Pesa Kibubu inaenda kubadilisha maisha yao.

Bwana Hamis Omary, Dereva Bodaboda

Tukianza na Bwana Hamis Omary Dereva Bodaboda ameelezea ni kwa namna gani huduma hii ya Tigo Pesa Kibubu inaenda kumtimizia ndoto yake ya kununua pikipiki mpya

“Pikipiki nayoiendesha sasa hivi ni ya mkataba ndoto yangu kubwa ni kumiliki pikipiki yangu mwenyewe hapo mwanzo nlikua nkiweka akiba ya kuifikia ndoto zangu kwa njia zisizo rasmi kama vile kuweka kwenye vibubu vya kienyeji au kuficha chini ya godoro suala ambalo limenikwamisha kwa mda maaana mda mwingine pesa zimekua zikipungua bila kuelewa zinaenda wapi au mda mwingine mekua nkishawishika kuzitumia, lakini Ujio wa TIGO PESA KIBUBU naona unaenda kunitimizia ndoto zangu , naifurahia Tigo Pesa Kibubu maana naweka akiba yangu kirahisi tena Kidigital”. Alimalizia Bwana Hamisi

Bwana Ally Juma Omary, Mfanyabiashara wa Mitumba

Kwa upande wake Bwana Ally Juma Omary mfanyabiashara wa Mitumba ambaye pia ni mpangaji ameeleza kwa namna ambavyo Tigo Pesa Kibubu itampunguzia kero na mwenye nyumba maana kwa sasa atakua akiweka akiba kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa Kibubu itakayomwezesha kulipa pesa ya Pango kwa wakati.

Kumbuka akaunti ya Tigo Pesa Kibubu itakuwa tofauti na akaunti yako kuu ya Tigo Pesa.

Ni rahisi sana kuweka akiba kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa Kibubu, Piga 15001#
●Chagua Huduma za kifedha (7)
●Chagua Akiba (8)
●Chagua TigoPesa Kibubu (1)
●Chagua weka akiba(1) na kisha weka kiasi na namba ya siri ya TigoPesa yako.

Kwa wateja wetu wanaotumia Tigo Pesa App, wanachotakiwa kufanya ni
Fungua Huduma za Kifedha
●Chagua Akiba
●Chagua Kibubu
●Chagua kuweka akiba na kisha weka kiasi na namba yako ya siri.

Huduma hii ni kwa kila mtumiaji wa Tigo Pesa, kuhamisha fedha kutoka Akaunti Kuu ya TigoPesa kwenda kwa Akaunti ya Kibubu ni BURE.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »