TANZANIA NA BURUNDI ZAENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA KILIMO-WAZIRI MKENDA

TANZANIA NA BURUNDI ZAENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA KILIMO-WAZIRI MKENDA

. Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Burundi Tanzania ina uhusiano mzuri na majirani wake na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa mshiriki kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhilishi wa migogoro kwa njia ya amani. Tanzania ni mwanachama wa vikundi vya kimataifa na kikanda pia inashiriki kwa dhati katika ushirikiano wa baina ya nchi na

Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakikagua viazi lishe vinavyozalisha na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu kwa ajili ya utafiti, Tarehe 20 Oktoba 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakipata maelezo kuhusu maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu inayotumika kwa ajili ya utafiti wa mazao ya kilimo, Tarehe 20 Oktoba 2021

Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakikagua mashamba ya viazi lishe vinavyozalisha na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu kwa ajili ya utafiti, Tarehe 20 Oktoba 2021

Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakikagua mashamba ya viazi lishe vinavyozalisha na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu kwa ajili ya utafiti, Tarehe 20 Oktoba 2021

.

Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakikagua baadhi ya mazao ambayo yamefanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu, Tarehe 20 Oktoba 2021

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Burundi

Tanzania ina uhusiano mzuri na majirani wake na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa mshiriki kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhilishi wa migogoro kwa njia ya amani.

Tanzania ni mwanachama wa vikundi vya kimataifa na kikanda pia inashiriki kwa dhati katika ushirikiano wa baina ya nchi na ushirikiano wa kimataifa.

Tanzania pia ilisaidia mazungumzo ya amani kumaliza mgogoro nchini Burundi ambapo mazungumzio hayo yalifanyika Jijini Arusha.

Serikali ya Tanzania imeendelea na juhudi zake za kuimarisha ushirikiano na nchi jirani ikiwemo Burundi ambapo pamoja na mambo mengine imekusudia kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo.

Kufuatia ushirikiano huo Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara ya kikazi nchini Burundi ambapo aliwasili Tarehe 18 Octoba 2021 na kuanza ziara ya siku mbili tarehe 19-20 Octoba 2021.

Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo Waziri Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide ambapo kwa kauli moja wamekubaliana kuendeleza ushirikiano maradufu.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Ngozi na Kayanza alipotembelea kujionea mashamba ya Kilimo cha mahindi (Block Farming) pamoja na kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu, Waziri Mkenda amesema kuwa lengo la ziara yake katika maeneo hayo ilikuwa ni kujionea hali ya ubora wa mazao ya wakulima yanayotumia mbolea ya FOMI.

“Tumekutana na wanasayansi wa hapa Burundi ili kuzungumza nao waweze kutueleza kuhusu utafiti walioufanya wa mbolea ya FOMI ili kujiridhisha kabla ya kuingia makubaliano ya kuanza matumizi ya mbolea hiyo kule nchini kwetu” Amekaririwa Waziri Mkenda

Waziri Mkenda amemuhakikishia mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide kuwa atampatia mualiko ili aweze kutembelea Tanzania kwa ajili ya kujifunza kuhusu kilimo cha mazao mbalimbali na kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Amesema kuwa viongozi wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Burundi wamekuwa wakijenga uhusiano mzuri wa Kidiplomasia na kisiasa kwani wananchi wameendelea kufanya biashara za mazao bila vikwazo hususani mazao ya mahindi, mchele na Parachichi.

“Tuna kazi kubwa sisi kama serikali kuimarisha mahusiano makubwa ya kibiashara na uchumi kama ambavyo viongozi wetu wanafanya, nasi tumekubaliana kushirikiana katika sekta ya utafiti wa mazao” Amesisitiza Waziri Mkenda

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »