SIMBA ‘OUT’ KLABU BINGWA

SIMBA ‘OUT’ KLABU BINGWA

Klabu ya @simbasctanzania imeondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha Mabao 3-1 toka kwa Klabu ya Jwaneng Galaxy ya Nchini Botswana katika mechi ya marudiano iliyochezwa katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 24, 2021. Simba waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na matumaini makubwa kufuzu hatua ya makundi

Klabu ya @simbasctanzania imeondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha Mabao 3-1 toka kwa Klabu ya Jwaneng Galaxy ya Nchini Botswana katika mechi ya marudiano iliyochezwa katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 24, 2021.

Simba waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na matumaini makubwa kufuzu hatua ya makundi wakiwa na mtaji wa magoli 2 baada ya ushindi walioupata katika mchezo wao wa awali na Jwaneng nchini Botswana na kuibuka na ushindi wa Magoli 2-0.

Baada ya Matokeo hayo timu zote mbili zinakuwa na jumla ya Pointi 3 na magoli matatu lakini Jwaneng Galaxy wanapata faida ya magoli matatu ya ugenini hivyo wanafuzu hatua ya makundi huku Simba wakielekea kushiriki Kombe la Shirikisho.

Magoli yote katika mchezo wa leo yalifungwa kama ifuatavyo, Simba SC 1-3 Jwaneng Galaxy (Bwalya 40’) (Rudath 46’ 59’ Mohutsiwa 85’)

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »