WAZIRI DKT. GWAJIMA AZIPA SALAMU ‘DAY CARE’ ZISIZOSAJILIWA

WAZIRI DKT. GWAJIMA AZIPA SALAMU ‘DAY CARE’ ZISIZOSAJILIWA

Na Mwandishi Wetu Dodoma Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewatumia salamu wamiliki wa vituo vya kulelea watoto mchana ambao hawajasajili vituo hivyo na wanaendelea kutoa huduma hiyo. Waziri Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo jijini hapa wakati wa Tamasha la Karibu Dodoma linalofanyika katika viwanja vya Chinangali

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewatumia salamu wamiliki wa vituo vya kulelea watoto mchana ambao hawajasajili vituo hivyo na wanaendelea kutoa huduma hiyo.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo jijini hapa wakati wa Tamasha la Karibu Dodoma linalofanyika katika viwanja vya Chinangali kwa siku sita tangu tangu Oktoba 24 na litakamilika Oktoba 29 mwaka 2021.

Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa Serikali haitovumilia kuona watu wanaanzisha na kuendesha Vituo vya kulelea watoto mchana bila kusajiliwa kwani kuna miongozo na namna za uendeshaji wa vituo hivyo unaotolewa na Serikali baada ya kusajiliwa vituo hivyo.

“Niwape tu salama ndugu zangu wale mlioanzisha vituo vya kulelea watoto mchana, nikija kukagua vituo hivyo tusikimbiane. Nitakuja kuanzia Desemba mwaka huu semeni ukweli tu hujasajiliwa ili upate elimu uelewe usajili kituo chako” alisisitiza Waziri Dkt. Gwajima

Wakati huo huo Waziri Dkt. Gwajima amewataka wazazi na walezi nchini kuzingatia suala la malezi kwa watoto kwani ni jambo la msingi na linasaidia kuondokana na matatizo mengi ikiwemo watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani.

Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa kuna wimbi la watoto wengi wanaokimbilia mitaani wanaotoka katika familia ikiwemo kukosa malezi, matatizo ya kifamilia na hata kunyang’anywa haki zao katika jamii kutokana na vifo vya wazazi au walezi wao.

Ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi na huduma muhimu zikiwemo elimu na afya huvyo wazazi na walezi wana wajibu wa kuhakikisha wanawapa malezi na matunzo stahiki watoto wao ili kuepukana na tatizo la watoto kukimbilia mitaani.

“Hii ni Wizara yangu nitahakikisha miongozo iliyopo hasa kuhusu watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani inatekelezwa kwa kupatikana mbinu sahihi ya kuwakusanya watoto na  kuwaunganisha na familia zao na wale ambao hawana familia wanapata familia za kuwalea kwa njia ya kuasili” alisema Waziri Dkt. Gwajima

Aidha Waziri Dkt. Gwajima amewataka watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kutowakimbia watu wanaotaka kuwasaidia na kuwaunganisha na familia zao au kuwatafutia familia za kuwalea kwani ni njia ya kuwasaidia kuondokana na madhira ya kuishi na kufanya mitaani.

Aidha, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kushirikiana na wadau mbalimbali katika maeneo yao kuwatambua watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani na kuwapatia msaada ili kuondokana na tatizo hilo katika mameno yao na kufanya watoto waishi katika mazingira salama na rafiki.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweli amesema kuwa Wilaya ya Dodoma itashirikiana na Wizara kuhakikisha inaweka utaratibu sahihi wa kuwatambua na kuwaunganisha familia zao, watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ikiwemo kuweka utaratibu mzuri wa kuwa na eneo litakalotumika kuwakusanya. 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeshiriki tamasha la Karibu Dodoma huku ikishirikisha Taasisi zake zote mbazo zilimetoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na mikoa ya karibu zikiwemo huduma za uchunguzi wa macho, moyo na matibabu ya kibingwa

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »