Mwaka 1 madarakani Rais Dkt Mwinyi amegawa Pesa kwa makundi yote Zanzibar.

Mwaka 1 madarakani Rais Dkt Mwinyi amegawa Pesa kwa makundi yote Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. HusseinAli Mwinyi amesema ili Taifa liweze kufanikisha matarajio ya kukuzaUchumi katika mwaka wa Pili wa Uongozi wa Serikali ya Awamu yanane, halina budi kuendelea kudumisha amani, uwajibikaji pamoja nawatendaji kujenga uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.Dk. Mwinyi ametoa indhari hiyo katika Hotuba aliyotoa kwa wananchi

May be an image of 2 people and text that says 'Kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi Septemba 2021, makusanyo yamekuwa jumla ya TZS bilioni 710.84 sawa na asilimia 69 ya makadirio ya kukusanya TZS bilioni 1,023.56. Makusanyo hayo ni ongezeko la asilimia 24 ikilinganishwa na makusanyo ya TZS bilioni 572.61 kwa kipindi cha Novemba 2019 hadi Septemba 2020. Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. CUNNTANANT ፍነንል MWAKA MMOJA YA AMANI NA WETU, SAFARI YA UJENZI WA UCHUMI MPYA INAENDELEA. NOVEMBA, 2021'


May be an image of one or more people and text
May be an image of ‎one or more people and ‎text that says '‎SEKTA YA ELIMU Tumeamua kuelekeza TZS. bilioni 69.0 kwa ajili ya kuzifanyia kazi changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. Serikali itakamilisha ujenzi wa madarasa 425 yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi, Shughuli hii tagharimu TZS bilioni 7.656. Tumepanga kujenga madarasa mapya 706 katika Wilaya zote 11 Unguja na Pemba kwa ngazi ya Maandalizi, Msingi na sekondari. AHIS CANDR Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. MWAKA MMAJA AMANI NA WETU, SAFARI YA UJENZI WA UCHUMI MPYA NAENDELEA. NOVEMBA, 2021 שיטיטיטיש GOLDEN TULIP AIRPORT HOTEL‎'‎‎
May be an image of one or more people and text that says 'Serikali imeamua kwa makusudi kuiboresha kwa kuipatia vifaa vya kisasa na madaktari wataalamu wa kutosha Hospitali ya Abdalla Mzee iliopo Mkoani Pemba na kuipandisha hadhi kuwa ni Hospitali ya Mkoa ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini na Kisiwa cha Pemba kwa ujumla. Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. MWAKA MMOJA YA AMANI NA WETU, SAFARI YA UJENZI WA UCHUMI MPYA INAENDELEA. NOVEMBA, 2021'
May be an image of 2 people and text
May be an image of one or more people and text that says 'UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI Wananchi wanaojishughulisha na kazi za mikono wakiwemo wahunzi, watu wenye ulemavu, wachoraji hina, watengenezaji wa mabango, mafundi gereji na ufinyanzi, wao tumewatengea jumla ya TZS bilioni 5.075 ambazo zitawanufaisha wananchi wapatao 22,600 Unguja na Pemba. AOD jumla wafanyabiashara wa maduka ya reja na jumuiya za masokoni, makundi haya yametengewa jumla ya TZS bilioni 5.2 ambapo tunatarajia kwamba zitawanufaisha jumla ya watu 950 Unguja na Pemba. Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. MWAKA MMNJA AMANI WETU, SAFARI YA UJENZI WA UCHUMI MPYA INAENDELEA. NOVEMBA, 2021 GOLDEN TULIP AIRPORT HOTEL'
May be an image of one or more people and text
May be an image of 5 people and text
May be an image of one or more people and text
May be an image of 2 people and text that says 'UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI Wananchi wanaojishughulisha na kazi za mikono wakiwemo wahunzi, watu wenye ulemavu, wachoraji hina, watengenezaji wa mabango, mafundi gereji na ufinyanzi, wao tumewatengea jumla ya TZS bilioni 5.075 ambazo zitawanufaisha wananchi wapatao 22,600 Unguja na Pemba. AOD jumla wafanyabiashara wa maduka ya reja na jumuiya za masokoni, makundi haya yametengewa jumla ya TZS bilioni 5.2 ambapo tunatarajia kwamba zitawanufaisha jumla ya watu 950 Unguja na Pemba. Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. MWAKA MMNJA AMANI WETU, SAFARI YA UJENZI WA UCHUMI MPYA INAENDELEA. NOVEMBA, 2021 GOLDEN TULIP AIRPORT HOTEL'
May be an image of one or more people and text that says 'UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI Wananchi wanaojishughulisha na kazi za mikono wakiwemo wahunzi, watu wenye ulemavu, wachoraji hina, watengenezaji wa mabango, mafundi gereji na ufinyanzi, wao tumewatengea jumla ya TZS bilioni 5.075 ambazo zitawanufaisha wananchi wapatao 22,600 Unguja na Pemba. AOD jumla wafanyabiashara wa maduka ya reja na jumuiya za masokoni, makundi haya yametengewa jumla ya TZS bilioni 5.2 ambapo tunatarajia kwamba zitawanufaisha jumla ya watu 950 Unguja na Pemba. Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. MWAKA MMNJA AMANI WETU, SAFARI YA UJENZI WA UCHUMI MPYA INAENDELEA. NOVEMBA, 2021 GOLDEN TULIP AIRPORT HOTEL'

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi amesema ili Taifa liweze kufanikisha matarajio ya kukuza
Uchumi katika mwaka wa Pili wa Uongozi wa Serikali ya Awamu ya
nane, halina budi kuendelea kudumisha amani, uwajibikaji pamoja na
watendaji kujenga uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Dk. Mwinyi ametoa indhari hiyo katika Hotuba aliyotoa kwa wananchi katika
kilele cha maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja wa Uongozi wake, hafla
iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliopo Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Amesema katika mwaka wa Pili wa Uongozi wa Awamu ya Nane, Serikali
imekopa jumla ya Shilingi Bilioni 460 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF)
ambazo shiligni Bilioni 230 kati ya fedha hizo zitatumika kufanikisha miradi
katika sekta mbali mbali za kijamii, ikiwemo Afya, elimu, maji safi na
salama na umeme pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Alisema Shilingi Bilioni 230 zilizobaki zitatumika kwa ajili ya kulipia madeni
ya Wazabuni, kulipa fidia mbali mbali pamoja na kulipia haki mbali mbali za
wafanyakazi.
Alisema fedha hizo (bilioni 230) zitakazoingizwa katika shughuli za
kiuchumi ni nyingi sana na ni wazi kuwa zitaleta faida kubwa kwa Taifa
pamoja na kurahisha maisha kutokana na mzunguko wa fedha.
Hivyo, alisema matarajio hayo yatakamilika tu endapo wananchi
wataendelea kudumisha amani iliopo, sambamba na watendaji kuanzia
ngazi za chini za uongozi kuwajibika ipasavyo na kufanya kazi zao kwa
uadilifu, hususan katika suala la tenda.

Alieleza kuwa katika kipindi kilichopita miradi mingi ilishindwa kukamilishwa
vyema kwa sababu ya Rushwa na kubainisha viashiria vilivyoanza
kujichomoza na kusisitiza kwamba yeyote atakaejaribu kuchota fedha hizo
hatomuachia.
Rais Dk.Mwinyi alitoa indhari juu ya matumizi stahiki ya fedha hizo, huku
akiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji wote
watakaojihusisha na udokozi au upotevu wa fedha hizo.
Katika hatua nyengine, Dk. Mwinyi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa
alizochukua kufanikisha kupatikana kwa mkopo huo pamoja na ukaribu
wake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao umekuwa chachu ya
kuondokana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza.
Aidha, Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imefanya uamuzi wa kuwalipa fedha zao (kiasi cha Shilingi Bilioni 38.7)
wahanga wote wa iliokuwa Masterlife, ikiwa ni hatua ya kuwaondolea
usumbufu wa maisha wananchi masikini walioweka fedha hizo.
Kitengo cha habari,
Ikulu Zanzibar

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »