Muigizaji Nyota wa Filamu za Kihindi, Sanjay Dutt kuitangaza Zanzibar kimataifa.

Muigizaji Nyota wa Filamu za Kihindi, Sanjay Dutt kuitangaza Zanzibar kimataifa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza ujio pamoja na azma ya Muigizaji Nyota wa Filamu za Kihindi, Sanjay Dutt ya kutaka kuekeza sambamba na kuwa Balozi wa kuitangaza Zanzibar kiutalii. Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi hizo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Muigizaji Nyota

May be an image of 4 people and indoor
May be an image of 5 people, people sitting and indoor
May be an image of 11 people, people sitting and people standing

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza ujio pamoja na azma ya Muigizaji Nyota wa Filamu za Kihindi, Sanjay Dutt ya kutaka kuekeza sambamba na kuwa Balozi wa kuitangaza Zanzibar kiutalii.

Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi hizo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Muigizaji Nyota huyo wa Filamu za Kihindi, Sanjay Dutt ambaye amekuja kuitembelea Zanzibar na kueleza jinsi alivyovutika na vivutio mbali mbali vilivyo Unguja na Pemba.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi pia, alimpongeza Nyota huyo kwa kueleza lengo lake la kuanzisha Kampuni yake hapa Zanzibar ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha tasnia ya Filamu hapa nchini sambamba na kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii Kimataifa.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba azma ya nguli huyo ya kuekeza Zanzibar katika sekta za maendeleo zikiwemo afya, elimu na nyenginezo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo lililowekwa na Serikali ya Awamu ya Nane la kuwarahisishia wananchi kupata huduma muhimu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »