RAIS DK.MWINYI AMEFUNGUA MADRASAT MARYAM ILIOPO MFENESINI WILAYA MAGHARIBI A UNGUJA

RAIS DK.MWINYI AMEFUNGUA MADRASAT MARYAM ILIOPO MFENESINI WILAYA MAGHARIBI A UNGUJA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. HusseinAli Mwinyi amesema kuna umuhimu wa jamii kuwatunza walimu wamadrasa kwa kuandaa mpango maalum wa kuwawezesha iliwahamasike katika ufundishaji , ikiwa pia ni hatua ya kuondokana naudhalili wa maisha walionao hivi sasa.Dk. Mwinyi ametoa wito huo Mfenesini katika hafla ya ufunguzi waMadrasatu Maryamu iliofanyika Mfenesini

RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  akisalimiana na kuagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh. Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Wadi, baada ya kumalizia hafla ya ufunguzi wa Masjid Tawba Kisauni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na  Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 8-10-2021.(Picha na Ikulu)    
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifungua mlango wa Masjid Tawba Kisauni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja baada ya kukata utepe kuufungua rasmin leo 8-10-2021, na kujumuima na Wauminin wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo.(Picha na Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi amesema kuna umuhimu wa jamii kuwatunza walimu wa
madrasa kwa kuandaa mpango maalum wa kuwawezesha ili
wahamasike katika ufundishaji , ikiwa pia ni hatua ya kuondokana na
udhalili wa maisha walionao hivi sasa.
Dk. Mwinyi ametoa wito huo Mfenesini katika hafla ya ufunguzi wa
Madrasatu Maryamu iliofanyika Mfenesini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema kuna umuhimu wa kuwatunza walimu wa madrasa ili
waweze kupata utulivu na kuwafundisha vyema wanafunzi, huku
akitilia mkazo kuwepo mipango ya kuwawezesha ili kuondokana na
maisha duni waliyonayo.
Aliwataka walimu na wazazi kuwahimiza watoto kudurusu masomo
yao ili waweze kufanikiwa, huku akiunga mkono juhudi za Madrasa
hiyo za kutoa msukumo katika ufundishaji wa muda wa ziada,
hususan kwa wanafunzi wanaokabiliwa na mitihani ya Taifa ya
mwisho wa mwaka.
Alisema serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa ya kusomea katika skuli Unguja na Pemba, ikiwa ni hatua
ya kukabiliana na mlundikano wa wanafunzi uanosababisha kuwepo
mikondo miwili ya masomo, hatua inayochangia wanafunzi kukosa
muda wa kwenda madrasa kusoma masuala ya Dini.
Aidha, aliutaka Uongozi wa Madrasa hiyo kuunda kamati
kushughulikia uendeshaji wa Madrasa, ambapo pamoja na mamabo
mengine itashughulikia suala la usafi.

Rais Dk. Mwinyi alisema mfadhili wa ujenzi huo tayari ametelekeza
wajibu wake, hivyo akawataka waumini wengine kujitokeza
kuendeleza ujenzi huo, akibainjisha wajibu huo kuwa ni wa watu wote
na sio wa wafadhili pekee.
Vile vile, alisiitiza umuhimu wa waumini kutoa sadaka kutoka
miongoni mwa yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu, kwa kigezo
kuwa suala hilo limeelezwa katika Qoraan na hadithi za Mtume
Muhammad (SAW) , huku akiwataka kutumia vyema majengo ya
Ibada.
Dk. Mwinyi aliwapongeza wahisani na watu wote waliotabaruki kwa
njia mbali mbali na hatimae kufanikisha ujenzi huo.
Aliahidi kuchangia upatikanaji wa Computa pamoja na kuahidi
kushirikiana na wafadhili mbali mbali kufanikisha ujenzi wa Ukumbi
wa Mikutano wa madrasa hiyo.
Nae, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab alisema suala
la ufunguzi wa madrasa sio kuwa ni la utamaduni wa Zanzibar, bali ni
dini iliorithiwa na Mtume Muhammad (SAW) pamoja na masahaba
zake.
Mapema, Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume,
akitoa salamu za Ofisi ya Mufti alisisitiza na kushajihisha usomaji wa
Qur-an, huku akifafanua kuwepo kheri , fadhila na ujira mkubwa kwa
walimu wa Qur-an, wanafunzi, waumini wanaosikiliza, wazazi wa
wanafunzi, wajenzi wa madrasa, pamoja na wale wanaofungua
madrasa hizo.
Aliitaka jamii ya Wazanzibari kuwapa heshima wanayostahili walimu
wa madrasa ikiwa ni hatua ya kuondokana na udhalili uanowakabili
hivi sasa.
Alisema Ofisi ya Mufti imeandaa masomo ya walimu wa madrasa ili
kuwasaidia namna ya ufundishaji na njia za kuwaadabisha wanafunzi
pale wanapokosea.
Akisoma Risala ya Madrasa hiyo Sheikh Suleiman Mohamed Omar
alisema miongoni mwa changamoto inazokabiliana nazo Madrasa

hiyo ni pamoja na uzito wa Wazazi katika kuchangia ada za mwezi
pamoja na mashirikiano madogo kati ya walimu na wazazi.
Madrsatul Maryamu yenye wanafunzi wapatao 1091, iliasisiwa mwaka
1995 na Bi Maryamu Mohamed Omar Ziwani kisiwani Pemba, ambapo
ujenzi wa Madrasa hiyo ya kisasa ya ghorofa mbili , unahusisha
vyumba 22, Ofisi ya walimu, maktaba pamoja na Chumba cha
Komputa ulianza mwaka 2005 kupitia kwa wafadhili mbali mbali.
Katika hafla hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alitembelea madarasa ya zamani ya
Madrsa hiyo pamoja na kuwakabidhi vyeti wnaafunzi sita waliohitimu
Juzuu 30.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »