Rais Samia amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118.

Rais Samia amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 22 Novemba, 2021 amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 02/18 wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi  na kundi la 08/18 Jeshi la Anga, katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 22 Novemba, 2021 amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 02/18 wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi  na kundi la 08/18 Jeshi la Anga, katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi (TMA) Monduli, mkoani Arusha.

Akitoa maelezo ya sherehe hizo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Brig.  Jen. Jackson Mwaseba amesema kati ya Maafisa hao wanafunzi waliohitimu 62 ni wa shahada ya Sayansi ya Kijeshi inayotolewa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa kushirikiana na Chuo cha TMA na 56 ni wahitimu wa mafunzo ya Urubani.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo amemshukuru Mhe. Rais Samia na Serikali kwa jitihada anazozifanya kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutekeleza kwa ukamilifu majukumu yake.

Aidha, Jen. Mabeyo amewapongeza Maafisa hao wapya kwa kuhitimu mafunzo yao kwa viwango vinavyokubalika na kuwakumbusha kuheshimu, kuthamini, kuzingatia na kutunza kiapo cha Utii walichoapa mbele ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Jen. Mabeyo amewataka Maafisa hao wapya kuwafundisha wafuasi wao maadili mema na kuwa macho na matishio ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na Majenerali, Maafisa, Askari na Wageni waalikwa Mhe. Rais Samia amekipongeza Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) na Chuo cha Uhasibu Arusha kwa ubunifu walionyesha katika kutoa mafunzo hayo kwa Maafisa hao wapya wa JWTZ.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewapongeza pia Wahitimu wote wa mafunzo hayo ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa kufuzu mafunzo yao.

Pamoja na kutunuku Kamisheni, Mhe. Rais Samia ametoa zawadi kwa Maafisa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi na kuwavisha mabawa Maafisa wapya wawili kwa niaba ya wenzao ikiwa ni ishara ya kuhitimu mafunzo yao ya urubani.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na kukiwezesha Chuo cha Uhasibu Arusha kutoa mafunzo ya Shahada ya Usalama wa Kimtandao (Cyber Security).

Shereheza kuwatunuku Kamisheni Maafisa hao zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Fedha pamoja na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba. Wengine ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi kutoka mikoa mbalimbali.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »