TIGO PESA WAZINDUA PROMOSHENI YA “LIPA KWA SIMU , UWin KUHAMASISHA MALIPO KIDIGITALI

TIGO PESA WAZINDUA PROMOSHENI YA “LIPA KWA SIMU , UWin KUHAMASISHA MALIPO KIDIGITALI

Dar es Salaam, Jumanne, Novemba 23, 2021, Kampuni inayoongoza kwa Utoaji wa huduma za kidijitali, Tigo, kupitia huduma yake ya Lipa Kwa Simu, imezindua promosheni ya mwisho wa mwaka inayoitwa Lipa Kwa Simu, uWini, promosheni inayolenga kuhamasisha wateja wa Tigo pesa kutumia huduma ya malipo ya kidijitali. Kupitia Promosheni hii Watumiaji wote wa Tigo Pesa


Dar es Salaam, Jumanne, Novemba 23, 2021, Kampuni inayoongoza kwa Utoaji wa huduma za kidijitali, Tigo, kupitia huduma yake ya Lipa Kwa Simu, imezindua promosheni ya mwisho wa mwaka inayoitwa Lipa Kwa Simu, uWini, promosheni inayolenga kuhamasisha wateja wa Tigo pesa kutumia huduma ya malipo ya kidijitali.


Kupitia Promosheni hii Watumiaji wote wa Tigo Pesa watapata zawadi za pesa taslimu hadi TZS 1,000,000, vocha za zawadi na kurudishiwa 10% watakapotumia Lipa Kwa simu kulipia bidhaa au huduma kwa wafanyabiashara waliochaguliwa kote nchini.

Ikiwemo Ushindi wa Milioni 1 kila mmoja kwa wateja kumi watakao kuwa na Idadi kubwa zaidi ya Miamala ya Lipa kwa simu kwa kipindi kizima cha kampeni. Promosheni ya Lipa Kwa Simu, uWini itaanza tarehe 23 Novemba 2021 na kumalizika tarehe 7 Januari 2022.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Promosheni hii, Afisa Mkuu wa Biashara na Huduma za Kifedha TIGO PESA , Bi. Angelica Pesha alisema kuwa, “Promosheni hii inalenga kukuza matumizi ya malipo Kidigitali nchi nzima hasa kuelekea kipindi hiki cha sikukuu za Chrismas na Mwaka mpya. Tumedhamiria kuwazawadia wateja wetu waaminifu katika msimu huu wa sikukuu kwa kila malipo watakayofanya kupitia huduma ya Lipa Kwa Simu na Tigo Pesa ambapo watapata nafasi ya kujishindia zawadi za fedha taslimu, punguzo la 10% katika maeneo yaliyochaguliwa na zawadi za Vocha.”

“Kila mteja atakayeshiriki atapokea ofa kwa njia ya SMS inayomtaka kufikia idadi au kiwango fulani cha miamala kupitia Lipa Kwa Simu kulingana na wastani wa matumizi yake ya kila wiki, akifikia namba ya lengo aliyotengewa mteja atapata zawadi ya Vocha kuanzia Tsh 2,000 hadi Tsh 100,000 kwenye akaunti yake ya TIGOPESA papo hapo. Na Wateja 10 bora tu ambao wataongoza kwa kutimiza lengo kwa 50% watapata zawadi ya Vicha ya TSh 100,000 kila wiki. Alieleza Pesha.

Promosheni ya Lipa kwa Simu uWini itawawezesha wateja wote kulipa kwa urahisi kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara katika sekta zote kama vile; Sehemu za soko, vituo vya mafuta, migahawa, baa, hoteli, maduka makubwa, maduka ya dawa, maduka ya vifaa na mengine mengi.

Mteja , mfanyabiashara pia atapata fursa ya kupokea malipo yake kupitia huduma hii ya Lipa Kwa Simu. Tunawahimiza wafanyabiashara wetu wote kupokea malipo ya kidijitali kutoka kwa wateja wao msimu huu wa sikukuu ili kujijengea nafasi ya kushinda.

Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa Tigo Pesa na hakuna haja ya kujisajili.

Mteja atatakiwa kufanya yafuatayo

  1. Piga 15001#
  2. Chagua ‘5’ Lipa Kwa Simu,
  3. Chagua “1” Kwa Tigo Pesa
    Au lipa kwa kutumia Tigo Pesa App na ufurahie kufanya miamala kirahisi na salama kwa kutumia simu ya mkononi.

Wateja wanahimizwa kulipia bidhaa na huduma mbalimbali kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu wakati na mahali popote nchini Tanzania ili kujijengea nafasi ya kushinda hadi pesa Taslim milioni Moja kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »