SERIKALI YATOA KAULI ABIRIA ALIYEKUTWA NA KIRUSI KIPYA CHA CORONA ‘OMICRON’

SERIKALI YATOA KAULI ABIRIA ALIYEKUTWA NA KIRUSI KIPYA CHA CORONA ‘OMICRON’

Serikali imesema tayari imeanza kufuatilia kupitia vyombo vya ndani taarifa za uwepo wa abiria mmoja aliyerudi nyumbani (India) mwenye aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 ‘Omicron’ ambaye alitokea Tanzania. Imeeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa za Maabara Kuu ya Taifa mpaka sasa hawajabaini anuwai mpya ya Uviko-19 (Omicron). Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya

Serikali imesema tayari imeanza kufuatilia kupitia vyombo vya ndani taarifa za uwepo wa abiria mmoja aliyerudi nyumbani (India) mwenye aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 ‘Omicron’ ambaye alitokea Tanzania.

Imeeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa za Maabara Kuu ya Taifa mpaka sasa hawajabaini anuwai mpya ya Uviko-19 (Omicron).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu ufafanuzi wa abiria huyo na wito wa kuendelea kuchukua tahadhari.

Amesema kwa kushirikiana ubalozi wa Tanzania nchini India wanafuatilia ili kubaini ukweli wa jambo hilo na baadaye kuchukua hatua stahiki.

“Bado haijajulikana kama abiria huyu alitokea Tanzania moja kwa moja au alipita Tanzania kuelekea India. Pia haijulikania alipita wapi kabla ya kufika India,” amesema Profesa Makubi.

Amesema Maabara ya Taifa pia imekuwa ikichunguza mabadiliko ya kirusi (Gene sequencing) kwa kuangalia uwepo wa anuwahi mbali mbali zinazotokana na mabadiliko ya Uviko-19 ikiwemo anuwai mpya ya Omicron.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »