TIGO WADHAMINI MAONESHO YA BIASHARA ARUSHA 2021 ‘ARUSHA TRADE FAIR’.

TIGO WADHAMINI MAONESHO YA BIASHARA ARUSHA 2021 ‘ARUSHA TRADE FAIR’.

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidigitali ya nchini, Tigo Tanzania, imedhamini Maonesho makubwa ya biashara ya mwisho wa mwaka Arusha, yanayoendelea katika  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, tangu  Jumatatu ya tarehe 13 na yanatarajiwa kufungwa  Jumapili ya tarehe 19, 2021. Ikumbukwe kuwa Maonesho haya yanayohusisha biashara mbalimbali yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa, wa-kati

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidigitali ya nchini, Tigo Tanzania, imedhamini Maonesho makubwa ya biashara ya mwisho wa mwaka Arusha, yanayoendelea katika  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, tangu  Jumatatu ya tarehe 13 na yanatarajiwa kufungwa  Jumapili ya tarehe 19, 2021. Ikumbukwe kuwa Maonesho haya yanayohusisha biashara mbalimbali yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa, wa-kati na wafanyabiashara wadogo (wajasiriamali) kujitangaza na kufanya biashara hasa katika kipindi cha msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. 

Malengo mengine ya Maonesho haya ni kuwa sehemu moja ambapo wananchi wanaweza kujipatia mahitaji yao yote muhimu kimanunuzi wakati wa msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka. Lakini pia Ni matarajio kuwa uwepo wa bidhaa anuai kutoka kwa washiriki kutatoa nafasi hii muhimu kwa wanunuzi kupata bidhaa zote sehemu moja. Kufanyika kwa maonesho haya kwa wiki nzima kunalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuwa na muda wa kutosha wa kufanya biashara na vilevile kwa watembeleaji kuwa na muda mrefu zaidi kufanya manunuzi.

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid pia umechaguliwa kutumika kwa sababu ya umaarufu wake, eneo uliopo na urahisi wa kufikika kwake ambapo hata wageni kutoka nje ya Jiji la Arusha wanaweza kuufikia kwa urahisi. Maonesho haya yamepangiliwa kwa mfumo wa “Mitaa” ambapo bidhaa zinazofanana hukaa eneo moja linaloitwa ‘mtaa’ na kumrahisishia mtembeleaji kujua aina za bidhaa na wapi kwa kuzipata kirahisi

Mitaa hiyo ni Pamoja na Mtaa wa X-mas na Mwaka Mpya, Mtaa wa Shule, Mtaa wa Sola na Taa, Mtaa wa Fedha, Mtaa wa Mawasiliano  na Mtaa wa Ujasiri Ni Mali.

Ushiriki wa maonesho haya unafanyika kwa njia rahisi ambapo wafanyabiashara wanafanya usajili moja kwa moja kupitia tovuti ya maonesho ya www.arushaholidayfair.comAkizungumza katika Maonesho haya Meneja wa Tigo  Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya amesema kuwa “Tigo Tanzania inayo furaha kuwa mdhamini mkuu wa maonesho makubwa ya biashara Arusha 2021, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid,yanayojulikana kama Arusha Trade Fair 2021.Maonesho haya yanayohusisha biashara mbalimbali yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabishara wakubwa,wa-kati na wadogo kujitangaza na kufanya biashara.” 

Meneja Mauzo wa Tigo kutoka Arusha, Salim Shangweli, akimuonesha mkuu wa Wilaya ya Arusha,Said Mtanda,banda la Tigo katika maonesho ya biashara Arusha Trade fair,katika viwanja vya  Sheikh Amri Abeid

“Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kubuni bidhaa na huduma zinazo walenga wafanyabiashara moja kwa moja kupitia huduma yetu ya Lipa Kwa Simu, tumedhamiria kuhakikisha kila mfanyabiashara atakae kuwa na banda hapa katika maonesho anatumia huduma ya Lipa Kwa Simu. Lipa kwa Simu ni huduma ya kifedha ya kidijitali inayomfanya mfanyabiashara au taasisi kupokea fedha kutoka kwa wateja wanaotumia simu za mkononi.” Aliongezea Mainoya

Gharama za viingilio katika maonesho haya ni Shs. 1,000/- kwa kulipia kupitia huduma ya Lipa Kwa Simu ya tiGO ama Tshs. 2,000/- kwa kulipia kwa pesa taslim mlangoni. 

Wito unatolewa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kushiriki na kutembelea maonesho hili ili kujipatia bidhaa na huduma mbalimbali kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »