Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema moja katika Shabaha ya Serikali ya Zanzibar ni kuwapatia wazanzibari huduma bora za Afya..

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema moja katika Shabaha ya Serikali ya Zanzibar ni kuwapatia wazanzibari huduma bora za Afya..

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema moja katika Shabaha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia wananchi wake huduma bora za Afya na za uhakika. Mhe. Hemed alieleza hayo katika Ufunguzi wa Maabara ya Taasisi ya utafiti wa Afya pamoja na Jengo  la Ofisi za watatifi  huko Binguni

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema moja katika Shabaha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia wananchi wake huduma bora za Afya na za uhakika.

Mhe. Hemed alieleza hayo katika Ufunguzi wa Maabara ya Taasisi ya utafiti wa Afya pamoja na Jengo  la Ofisi za watatifi  huko Binguni Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema ili lengo hilo liweze kufikiwa hakuna budi kwa watendaji kuhakikisha huduma za uchunguzi wa maradhi katika maabara hiyo zinaboreshwa na kupewa kipaumbele hasa katika kuwajengea uwezo watendaji na kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya kisasa katika maabara hizo.

Makamu wa Pili wa Rais alieleza kuwa Maabara ya kisasa ya tafiti za Afya ni ya kipekee kwa hapa Zanzibar itakayofanya tafiti mbali mbali ikiwemo uchunguzi wa dawa za kitaamu zinazotumika pamoja na zile zinazotokana na mimea.

“Kadhalika kufutia uwepo wa UVIKO 19, maabara hii itatumika kufanya uchunguzi wa ugonjwa huu pamoja na maradhi mengine ya miripuko yanayoathiri jamii”. Alisema Makamu wa Pili

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Hemed alitoa wito kwa watumishi kuzitumia mashine zilizofungwa katika kituo hicho kwa umakini na uwangalifu wa hali ya juu kutokana na ghrama kubwa za vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.

Aidha, alitumia fursa hiyo kupongeza ushirikiano uliokuwepo kati ya taasisi hiyo ya utafiti na taasisi nyengine za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanzia kama  vile Taasisi ya utafiti na magonjwa ya binadamu (NIMR) na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) sambamba na mashirikiano yaliokuwepo kutoka kwa washirika wa maendeleo.

“Pia Nimefurahishwa kuskia tayari maafunzo maalum yametolewa ya matumizi ya mashine hizo kwa siku ishirini kwa wataalamu kumi na saba, Ahsanteni sana washika wetu wa maendeleo” Alieleza Mhe. Hemed

Nae, Waziri wa Afya ustawi wa jamii, wazee jinsia na watoto Mhe. Ahmed Nassor Mazurui alisema serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendeleza Shabaha yake ya Mapindizi Matukufu ya Zanzibar kwa kuhakikisha vituo mbali mbali vya Afya vinaendelea kujengwa ili kuwapatia huduma bora za masula ya Afya wananchi wake.

Alisema katika ujenzi wa taasisi hiyo ya Utafiti wa Afya kwa maabara iliopo Binguni zaidi ya Shillingi Millioni Mia tatu tisini na Moja zimeptolewa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Swiss Development Corporation ambayo imetoa zaidi ya Shillingi Millioni Mia moja Arubaini na Tano.

Waziri Mazurui alimueleza kuwa miongoni mwa tafiti zilizofanywa ni pamoja na kukamilika kwa tafiti ya nyungu kupitia miti mbali mbali iliosaidia watu kujifukiza kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya maradhi ya UVIKO-19.

Akitoa salamu kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Rashid Hadid Rashid alisema wananchi wa Mkoa wataendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kuiendeleza Taasisi hiyo ya Utafiti wa Afya kwa ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Kusini na Zanzibar kwa ujumla.

Mhe. Hadid alieleza kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia chini viongozi wake wa juu wakiongzwa na Rais Dk. Mwinyi wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika kuendelea kujenga hospìtal pamoja na vituo vya Afya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amezindua jengo la maabara  lenye vyumba vinane likiwa na vifaa vya kisasa vya kutendea kazi pamoja jengo kwa ajili ya Ofisi za watafiti wa taasisi ya utafiti wa Afya.

Uzinduzi wa Taasisi hiyo ni miongoni mwa Shmrashara za miaka Hamsini na nane (58) ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »