Rais Dkt. Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia.

Rais  Dkt.  Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia, ilioandaliwa maalum kwa ajili ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil, Kikwajuni jijini Zanzibar, ambapo magwiji wa sanaa ya muziki

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia, ilioandaliwa maalum kwa ajili ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil, Kikwajuni jijini Zanzibar, ambapo magwiji wa sanaa ya muziki wa Taarabu asilia kutoka Kikundi cha Taifa Zanzibar, walionyesha umahiri wao katika kuchararaza nyuzi na kughani nyimbo mbali mbali na kukonga nyoyo za mashabiki wa sanaa hiyo kutoka Mikoa yote ya Zanzibar.

Katika burudani hiyo nyimbo mbali mbali zilizopata kuvuma na kupendwa kutoka kwa watunzi wabobezi na waimbaji nguli wa sana hiyo zilipata fursa ya kuimbwa na kuibua vifijo na nderemo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »