TAMKO KUHUSU MAKAO YA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI YANAYOENDESHWA BILA LESENI NCHINI

TAMKO KUHUSU MAKAO YA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI YANAYOENDESHWA BILA LESENI NCHINI

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inatoa siku 30 tangu tarehe ya tamko hili hadi tarehe 18 Februari, 2022 kwa Makao ya watoto yasiyo na leseni kuwasilisha maombi ya usajili katika Halmashauri husika kuboresha huduma muhimu zinazohitajika katika makao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni.Hadi Januari 2022, Makao ya watoto 244 pekee


Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inatoa siku 30 tangu tarehe ya tamko hili hadi tarehe 18 Februari, 2022 kwa Makao ya watoto yasiyo na leseni kuwasilisha maombi ya usajili katika Halmashauri husika kuboresha huduma muhimu zinazohitajika katika makao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni.
Hadi Januari 2022, Makao ya watoto 244 pekee kati ya 473 ndiyo yaliyokidhi vigezo na kupata leseni kutoka kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii huku Makao 229 yakiendeshwa kinyume cha taratibu. Aidha, uendeshaji wa makao bila leseni ni kinyume na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009, pamoja na Kanuni zake. Hali hii inaweza kusababisha uwepo wa makao yasiyokidhi vigezo na usalama kwa watoto.


Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009, ikisomwa na Kanuni za Uanzishaji na Uendeshaji wa Makao ya Watoto za mwaka 2012, mtu yoyote anayekusudia kuendesha makao ya watoto atatakiwa kuomba leseni ya uendeshaji wa makao hayo kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii. Ikumbukwe kwamba ni kinyume cha sheria kutumia leseni moja kuendesha makao zaidi ya moja.


Serikali inatambua jitihada kubwa za wadau wanaolea watoto walio katika mazingira hatarishi katika makao ambao wanafuata sheria, taratibu na kanuni za ulinzi na usalama wa watoto wawapo vituoni.
Hivyo, nawaagiza waendeshaji wa makao ya watoto ambayo hayajasajiliwa kuhakikisha wanakidhi vigezo na kukamilisha taratibu za usajili ndani ya muda uliotolewa. Vilevile, natoa wito kwa Halmashauri zote nchini kupitia kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kufanikisha zoezi la ukaguzi wa makao ambayo hayajasajiliwa na yaliyokidhi vigezo na masharti ya utoaji wa huduma kwa mujibu wa sheria yaombewe usajili katika muda uliotolewa.

Aidha, Makao ambayo yatakuwa hayajaomba usajili baada ya muda uliotolewa hatua za kisheria zitachukuliwa.
Maelekezo ya Vigezo na Masharti ya usajili yanapatikana katika Ofisi za Ustawi wa Jamii zilizopo Halamshauri ya Mji, Wilaya, Manispaa na Majiji pamoja na kwa Maafisa Ustawi wa Jamii waliopo Ofisi za Kata.
Nawahimiza Wakurugenzi wote wa Halmashauiri nchini, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa kutoa ushirikiano katika kutambua makao yasiyosajiliwa na kutoruhusu makao ya watoto yasiyo na leseni, kuanzishwa katika maeneo yao. Aidha, Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali yanayomiliki makao yanaelekezwa pia kufuata utaratibu wa kupata leseni.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »