NUSU YA SIMBA WOTE DUNIANI WAKO TANZANIA.

NUSU YA SIMBA WOTE DUNIANI WAKO TANZANIA.

RAIS wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa, (SCI), Sven Lindqueast ameitaja Tanzania kuwa ni nchi yenye  nusu ya simba wote Duniani katika Mkutano wa 50 wa Mwaka wa Uwindaji wa Kitalii unaoendelea kufanyika nchini hapa. Rais huyo Bw. Sven Lindquest amesema kwa hatua hiyo ameipongeza kwa juhudi za utunzaji na kupelekea wingi wa wanyama hao.

RAIS wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa, (SCI), Sven Lindqueast ameitaja Tanzania kuwa ni nchi yenye  nusu ya simba wote Duniani katika Mkutano wa 50 wa Mwaka wa Uwindaji wa Kitalii unaoendelea kufanyika nchini hapa.

Rais huyo Bw. Sven Lindquest amesema kwa hatua hiyo ameipongeza kwa juhudi za utunzaji na kupelekea wingi wa wanyama hao.

Kwa upande wake Serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ametaja sababu zilizopelekea nchi ya Tanzania kutajwa kuwa nchi yenye Simba wengi Duniani licha ya kuruhusu uwindaji wa kitalii.

Akizungumza leo  katika  Jijini la  Las Vegas nchini Marekani, Dkt.Ndumbaro amesema nusu ya simba wote wapo Tanzania  kutokana na uimara wa serikali ya Tanzania katika shughuli za  uhifadhi

Amesema kuimarika kwa shughuli za uhifadhi hususani kwa Wanyamapori walao nyasi ni moja ya sababu ya Tanzania kuwa na Simba wengi  hivyo imepelekea  Simba nao  kuongezeka kutokana na uhakika wa  chakula cha kutosha 

Amefafanua kuwa Simba hula wanyamapori walao nyasi na wanyamapori hao walao nyasi wamekuwa wengi kutokana na uwepo wa nyasi za kutosha kutokana na usimamizi bora wa maeneo ya Hifadhi

” Kubadilishwa  mfumo kutoka wa kirai kwenda katika mfumo wa kijeshi kwa Watumishi wote wanaosimamia maeneo ya Hifadhi ni moja ya sababu ya simba kuongezeka kwa Simba nchini Tanzania” alisema Dkt.Ndumbaro

Waziri  Ndumbaro  amesisitiza kuwa Tanzania imefanikiwa kuwa simba wengi kutokana na serikali kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini kwa kuitengea Wizara ya Maliasili na Utalii bajeti ya kutosha inayotumika katika kuendesha operesheni mbalimbali za kukabiliana na ujangili

Amesema hadi sasa Serikali imeweza kufanikiwa kukomesha tatizo hilo la  ujangili kwa  zaidi ya asilimia 90 na kusisitiza kuwa ifikapo 2025 itarajia kumaliza kabisa tatizo la  ujangili kwa kufikia asilimia 100% 

” Uthubutu wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan wa kuwa bega kwa bega na Wizara imekuwa chachu kwa Tanzania kuzidi kuongoza kwa kuwa na simba wengi Duniani” amesisitiza Dkt Ndumbaro 

Pia, Dkt.Ndumbaro ameitaja sababu nyingine kuwa ni utolewaji wa elimu kwa Jamii,  amesema kwa sasa Jamii imetambua umuhimu wa wanyamapori hivyo wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa serikali  kwa kutoa taarifa vitendo vya ujangili vinapotokea. 

” Kama nchi tumejiwekea utaratibu wa kuhakikisha wananchi wote wanaoishi katika maeneo ya Hifadhi wananufaika kwa kusogezewa huduma za kijamii, hivyo Jamii imekuwa inaona faida ya moja kwa moja ya uwepo wa  wanyamapori” alisisitiza Dkt. Ndumbaro

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema  uwepo wa sheria kali ya  kutokuruhusu shughuli za kibinadamu kuendeshwa ndani ya maeneo ya Hifadhi kumepelekea maeneo ya Hifadhi kubaki katika uasili wake hivyo  simba wamezidi kuongezeka kutokana uwepo mazingira salama ya wanyamapori wengine

Aidha, Dkt.Damas Ndumbaro amesema licha ya Tanzania kuwa na vitalu vya uwindaji wa kitalii zaidi ya 100 lakini imekuwa  ikiendesha Uwindaji huo  kwa kuzingatia  matumizi  endelevu ndio maana imezidi kuongoza Duniani kwa kuwa na simba wengi 

Kufuatia hali hiyo, Dkt. Ndumbaro amekanusha madai ya baadhi ya nchi zinazopinga  Uwindaji wa Kitalii kwa kisingizio kuwa utalii huo umekuwa ukipunguza idadi ya wanyamapori ambapo amesisitiza kuwa Uwindaji wa Kitalii ni muhimu kwa kuwa umekuwa ukisaidia kupunguza idadi ya wanyamapori waliozidi ili kupunguza athari kwa binadamu

Amesema kwa sasa nchini Tanzania kumekuw athari kwa binadamu kutokana na ongezeko la  Wanyamapori kama vile tembo pamoja na mamba.

Na Mwandishi Maalum, Las Vegas,Marekani.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »