MAJALIWA: RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUIFUNGUA TANZANIA.

MAJALIWA: RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUIFUNGUA TANZANIA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuifungua Tanzania kwa kujenga barabara katika maeneo mbalimbali nchini ili Watanzania wazitumie katika kufanya shughuli kijamii zikiwemo biashara. Aliyasema hayo jana (Jumatatu, Januari 24, 2022) alipozungumza na wananchi wa Dareda akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani Manyara.

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASSIM MAJALIWA .


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuifungua Tanzania kwa kujenga barabara katika maeneo mbalimbali nchini ili Watanzania wazitumie katika kufanya shughuli kijamii zikiwemo biashara.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu, Januari 24, 2022) alipozungumza na wananchi wa Dareda akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani Manyara.

Alisema kuwa Serikali ipo katika mpango wa ujenzi wa barabara za Mbulu-Hydom, Karatu-Mbulu, Hydom Mkalama-Sibiti-Meatu-Bariadi-Maswa hadi Busega

“Barabara zote hizi zinatakiwa kuwekwa lami ili mzitumie fursa hizi kufanya biashara na kusafiri kwa urahisi, leo hii tunajenga makao makuu ya Halmashauri ya Mbulu pale Dongobesh, hivyo tunajenga barabata kutoka Dongobesh kuja hapa Dareda Centre ili halmashauri ifikike kwa urahisi”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwaondoa hofu wananchi wote waliolipia huduma ya kuunganishiwa umeme ambao bado hajapata huduma hiyo kuwa wataunganishiwa kwani tayari wakandarasi wameshapelekwa katika maeneo yao.

“Watu wote waliolipia na watakaolipia huduma ya kuunganishiwa umeme wataunganishiwa. Malengo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinapata umeme ifikapo Desemba mwaka huu.”

Akizungumzia kuhusu utunzaji wa mazingira, Mheshimiwa Majaliwa aliwasisitiza Watanzania watunze mazingira na wapande miti kwa wingi ili nchi iweze kupata mvua za kutosha. “Tusiruhusu watu kuharibu mazingira tutakosa maji, pandeni miti kwa wingi ili kuliepusha Taifa kugeuka kuwa jangwa.”

Alisema katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo mito iliyokuwa ikitiririsha maji inaanza kukauka kutokana na uharibifu wa mazingira, hivyo kusababisha kupungua kwa vyanzo vya maji.

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kuwapongeza kwa ubunifu mzuri kwani jengo lao ni la mfano. Jengo hilo hadi kukamilika linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 6.3.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMANNE, JANUARI 25, 2022.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »