MWALIMU ALIYEJITOLEA KUFUNDISHA KWA MIAKA 22.ANAJENGEWA NYUMBA KILOSA.

MWALIMU ALIYEJITOLEA KUFUNDISHA KWA MIAKA 22.ANAJENGEWA NYUMBA KILOSA.

WAFUGAJI jamii ya kimasai kijiji cha Twatwatwa wilayani kilosa wameadhimia kumjengea nyumba ya kuishi mwalimu Mariam Masud Sanya ambaye amejitolea kufundihsa wanafuzi kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 20 Mwalimu Sanya alisema kuwa alianza kufundisha kwa kujitolea tangu mwaka 2000 na baadaye kusomea ualimu wa memkwa mwaka 2003 elimu iliyomsaidia kufundisha wanafunzi wa shule za

WAFUGAJI jamii ya kimasai kijiji cha Twatwatwa wilayani kilosa wameadhimia kumjengea nyumba ya kuishi mwalimu Mariam Masud Sanya ambaye amejitolea kufundihsa wanafuzi kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 20

Mwalimu Sanya alisema kuwa alianza kufundisha kwa kujitolea tangu mwaka 2000 na baadaye kusomea ualimu wa memkwa mwaka 2003 elimu iliyomsaidia kufundisha wanafunzi wa shule za msingi

Alisema kwa kpindi chote hicho alikuwa akifundisha katika shule za msingi shikizi ambapo akianzia shule ta Twatwana na baada ya shule hiyo kupata usajili alihamia shule ya msingi shikizi ya Manyara kijijini hapo hadi kufikia mafanikio ya kufaulisha wanafunzi wa darasa la nne na darasa la saba

“nilianza kufundisha baada ya kupata elimu ya shule za awali mwaka 2000 baadae ndio nikajiendeleza kufundisha memkwa kwahiyo kwa kipindi chote nilikuwa nikifunsiaha shule ya msingi Twatwatwa na ilipo pata usajili ndio nikahamia hapa Manyara” alisema Sanya

Alisema alisema nmamo mwaka 2006 ndio alihamia shule ya msingi shikizi ya Manyala akianza na wanafunzi 20 ambao alikuwa akiwafundisha chini ya mti ambapo mpaka sasa yapata miaka 17 shule hiyo imefikisha idadi ya wanafunzi 118 ikiwa na madara 7

Alisema kwa kipindi chote anajivunia kuwafunisha wanafunzi haokutokana na uzoefu alioupata baada ya kupata semina za walimu wa awali na memkwa mara ya kusomea taaluma hiyo na kufanikiwa kufaulisha wanafunzi wake

“nashukuru sana viongozi wa kijiji kwa kutambua mchango wangu na kuamua kunijengea nyumba ambayo ameanza tayari hatua ya mwazo ambapo itanisaidia kwa siku za baadae” alisema

Mkuu wa wilaya ya kilosa Majid mwanga aliwapongeza wananchi hao kwa hatua hiyo ya kumjengea nyumba mwalimu Sanga nyumba ikiwa nikatika kutambua mchango wake alioutoa kwa wanfunzi kaytika kipindi chote alichofanya kazi

Alisema serikali itendelea kuwa bega kwa began a wananchi wa kijiji hicho katika kuwaletea maendela hasa katika sekta ya elimu ambapo kwa sasa baada ya kuongeza vyumba vitatu vya madarasa tayarwameshaongeza walimu wawili kwaajili ya kufundisha wanafunzi hao

“niwahakikishie serikali yenu ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suruhu Hassan itaendelea kuboresha miundombinu ya elimu kadri iwezekanyo, baada ya rasi kuwajengea madarasa mapya 3 akaona haitoshi sasa ameleta walimu wapya wawili akiemo mwalimu mkuu wa shule hii mpya” alisema Mwanga

Naye mbunge wa jimbo la kilosa Palamagamba kabudi aliahidi kuchangia ujenzi wa nyumba ya mwalimu huyo kiasi cha shilingi 500,000 na mkumtaka mwalimu mkuu mpya kumpa nafasi ya kufundisha mwalimu huyo pale inapohitajika

Alisema kutokana na uzoefu aliokuwa nao mwalimu huyo na mahusiano mazuli yaliyopo baina yake na wanafunzi ni vyema akaendelea kuwafundiha ili kuponguza changamot ya uhaba wa walimu katika shule hiyo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »