SERIKALI YA ZANZIBAR YAZIDI KUENDELEZA MIRADI YA MAENDELEO KUTATUA CHANGAMOTO

SERIKALI YA ZANZIBAR YAZIDI KUENDELEZA MIRADI YA MAENDELEO KUTATUA CHANGAMOTO

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahikikishia wananchi wa Zanzibar kuwa miradi ya maendeleo  inayoendelea kujengwa itapunguza changamoto mbali mbali  za kijamii zinazowakumba wananchi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua Miradi ya maendeleo inayojengwa na Serikali kwa fedha za ahueni za

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahikikishia wananchi wa Zanzibar kuwa miradi ya maendeleo  inayoendelea kujengwa itapunguza changamoto mbali mbali  za kijamii zinazowakumba wananchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua Miradi ya maendeleo inayojengwa na Serikali kwa fedha za ahueni za Uviko 19, katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema serikali imeamua fedha hizo kuzielekeza katika miradi ya kijamii, ambapo wananchi wa Zanzibar wanahitaji zaidi huduma hizo, ambapo kukamilika kwa miradi hiyo kutawapunguzia wananchi kufuata huduma hizo kwa masafa ya mbali na kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa wananchi wa eneo hilo, na maeneo jirani.

Amesema Kuwepo kwa Miradi hiyo kutatoa nafasi kwa serikali kusogeza huduma mbali mbali za kijamii, ikiwemo miundombinu ya barabara, maji na umeme ili kuwarahisishia wananchi  wanaofika kupata huduma katika maeneo hayo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaomba wakandarasi wanaosimamia miradi hiyo kutoa fursa kwa wananchi wa maeneo hayo kwa  kuwapatia ajira za muda ili wanufaike na miradi hiyo.

Kuhusu maeneo yanayopita miundombinu mbali mbali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka mamlaka husika kufanya utaratibu mzuri kwa kuondosha miundombinu hiyo ili kutoa nafasi kwa wakandarasi kuelea na ujenzi wa miradi hio.

Katika Ziara hiyo Mhe. Hemed amezitaka wizara husika zilizopata miradi kuhakikisha wanasimamia fedha hizo na kuhakikisha malengo ya fedha hizo yanafanikisa na kuwakabidhi wakandarasi wa miradi hio ili kuanza haraka kwa ujenzi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, wanawake na watoto pamoja na wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali kufanya tathmini juu ya maombi ya Wataalamu wa wizara hizo, ambapo amesema Hospital zitakuwa na madaktari Bingwa wanaoendana na hadhi na walimu waliobobea pamoja na kutoa ajira za kudumu kwa wataalamu hao.

Pia Mhe. Hemed ameeleza kuwa majengo yote yatakuwa navifaa na samani za kisasa ambazo zitaweza kurahisisha zaidi huduma kwa wananchi katika majengo hayo.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameendelea kuwataka wakandarasi walioamini kupewa miradi hiyo kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na iwe naviwango bora kama walivyokubaliana katika Mikataba ya makabidhiano.

Aidha Mhe. Hemed amewataka wananchi wa maeneo yaliyopata miradi hiyo kutoa mashirikiano ya kutosha ili kusaidia kukamilika miradi hiyo kwa wakati kwa manufaa ya wote.

Nae waziri wa elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Muhamed Said amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuelekeza fedha hizo katika miradi ya kujenga na kukarabati Skuli, jambo ambalo linawajengea Imani Wananchi kwa Serikali yao, na kumuhakikishia kuwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuendelea na miradi mengine iliyopangwa na Serikali.

Nao wakuu wa Wilaya ya Magharibi A na Wilaya ya Magharibi B, wamehukikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa wataendelea kushirikiana na wizara husika pamoja na wakandarasi ili kusimamia Miradi hiyo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wa maeneo yalionufaika na miradi hiyo viongzi wa majimbo wameishukuru Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dr Mwinyi kwa kuwafikishia miradi hiyo, ambapo kukamilika kwa miradi hiyo kutaweza kusaidia kumaliza Kilio cha wananchi katika uhaba wa Vituo vya Afya na uhaba wa Skuli, na kumuomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuangalia zaidi ujenzi wa barabara za ndani ili kupunguza changamoto ya miundombinu hiyo.

Ziara hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo Mhe.  Hemed amekagua ujenzi wa Hospital za Wilaya ndan ya Mkoa wa Mjin zilizopo Mwanakwerekwe Ijitimai, Chumbuni na Mbuzini, ujenzi wa Hospital ya Mkoa Lumumba,  ujenzi wa Skuli ya Mwanakwerekwe D na G,  Skuli ya sekondari mtopepo, na ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Masingini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »