JAJI Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahimu Juma amesema kuna haja ya kuboreshwa kwa mifumo ya TEHAMA ya Mahakama katika kusaidia wananchi katika utoaji huduma na kukuza uchumi hali hiyo inatokana na mifumo mingi ya Mahakama kuwa na changamoto yakutosomana na hivyo kutoleta manufaa kwa wananchi. Profesa Juma ametoa maelezo hayo leo Januari 27,2022 Jijini Dodoma mara
JAJI Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahimu Juma amesema kuna haja ya kuboreshwa kwa mifumo ya TEHAMA ya Mahakama katika kusaidia wananchi katika utoaji huduma na kukuza uchumi hali hiyo inatokana na mifumo mingi ya Mahakama kuwa na changamoto yakutosomana na hivyo kutoleta manufaa kwa wananchi.
Profesa Juma ametoa maelezo hayo leo Januari 27,2022 Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki maonesho ya wiki ya Sheria ambayo Kitaifa yanafa katika Viwanja vya Nyerere Skwea Jijini Dodoma.
Hata hivyo Jaji Mkuu amezungumzia kuhusu Sheria ya adhabu ya kunyongwa.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo akiwemo Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU Grabriella Gabriel,Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA,Lilian Mollel na Kaimu Katibu wa Tume ya marekebisho ya Sheria Nchini,Zainabu Chanzi wakaeleza huduma wanazozitoa katika wiki ya Sheria.
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa mwaka 2022 yanakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Dhama za Mapinduzi ya nne ya viwanda, na kilele ni Februari Mosi Mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *