WAWILI WAFARIKI AJALI YA LORI KIMARA, NANE WAJERUHIWA

WAWILI WAFARIKI AJALI YA LORI KIMARA, NANE WAJERUHIWA

Watu wawili wamefariki dunia papohapo na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyosababishwa na lori lililowafuata abiria katika kituo cha daladala Kimara Suka jijini Dar es Salaam. Akizungumzia ajali hiyo leo Ijumaa Januari 28, 2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo amesema watu hao walikuwa wakisubiri usafiri katika kituo

Watu wawili wamefariki dunia papohapo na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyosababishwa na lori lililowafuata abiria katika kituo cha daladala Kimara Suka jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ajali hiyo leo Ijumaa Januari 28, 2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo amesema watu hao walikuwa wakisubiri usafiri katika kituo hicho.

Amesema ajali hiyo iliyosababishwa na lori imehusisha na baadhi ya vyombo vingine vya usafiri ikiwemo daladala, bajaji na pikipiki.

“Watu wawili wamefariki dunia na wanane wamepata majeraha wengine wamepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wengine wamepelekwa Mloganzila,” amesema Kamanda Murilo.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Usalama wa Barabarani Taifa, ACP Abdi Isango ambaye aliyefika eneo la tukio amesema ajali hiyo imehusisha watu na vyombo vya usafiri.

Dk Mambo Meekson wa Hospitali ya Bochi iliyopo Kimara kwa Msuguri amethibitisha kupokea majeruhi watatu katika hospitali hiyo ambao ni wanawake.

“Ni kweli tumepokea majeruhi kutoka katika ajali ya Kimara Suka na tunaendelea nao kuwapa huduma katika kitengo cha dharura,”

“Majeruhi hawa wameletwa na wasamaria wema na hii imekuwa ikijitokeza wakiletwa tunawapatia matibabu badae tunawajulisha Polisi wanakuja na yote hiyo inatokana na hospitali yetu kuwa karibu na barabara hii, “amesema Dk Meekson

Shuhuda wa ajali hiyo, Juma Omary amesema lori hilo lilionekana kusogea kwa kasi na baadaye liliwavaa watu waliokuwa katika kituo cha daladala na wakiwemo madereva bodaboda.

“Ajali imetokea mapema sana saa 12 asubuhi, hapa ni kituoni na watu walikuwa wamesimama wengine wanasubiri kuvuka barabara na wengine wakisubiri daladala na kuna bodaboda walikuwepo hapa,” amesimulia shuhuda huyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »